Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

Kizazaa cha fedha za Kampeni Lowassa, CHADEMA na UKAWA


Kwa mujibu wa habari nyeti nilizotonywa sasa hivi kuna kizazaa cha fedha za kampeni zinazowafanya
Lowassa, Chadema na UKAWA kwa ujumla kuwa katika mtafuruku mkubwa na mpaka sasa uliopelekea kuchelewa kuanza uzinduzi wa kampeni ya Urais wa ukawa.

Vyama vinayounda UKAWA vinasema Lowassa aliahidi kuwa atatowa fedha zote za kampeni kwa hiyo wao wasiulizwe. Lowassa anasema alizotowa zinatosha (hasemi katowa kampa nani na za nini), Chadema nao wanavunga kuwa mpaka sasa akaunti ya kutowa kiasi kikubwa cha fedha ni lazima saini ya Katibu Mkuu iwepo na Katibu Mkuu wa chadema alipofatwa kusaini yeye kagoma ( huu ni ungo wa chadomo) wanasema eti Katibu Mkuu wao anataka kwanza taratibu za kubadili saini yake zikamilike kama watatowa fedha watowe wenyewe akikamilisha zoezi la kubadili kuwa ndiyo anawakwamisha.

Kizungumkuti kinaendelea wakati marafiki matajiri waliokuwa wanampa fedha azitakazo Lowassa wameona mambo yanakuwa magumu na badala ya fedha wameanza kumpa ahadi za kesho, kesho, kesho huku wakitazama upepo unapovuma.

Kuna habari nyingine kuwa kuanzia jana kuna ng'ombe zaidi ya 3,000 wanapakiwa wapelekwe sokoni kutoka kwenye ranchi moja kubwa sana iliyopo huko Handeni, sijuwi nayo inahusiana na Lowassa?

Kwa mujibu wa mtonyaji wangu anasema, Ndesamburo nae kagoma kutowa fedha, anasema Lowassa aliahidi atatowa fedha zote za kampeni yake yeye mwenyewe kwa hiyo asiulizwe yeye.

Mzee Mtei yupo mbioni kuwasiliana na Lowassa, Lowassa hapatikani kwa muda mrefu kwenye simu

Jamii Forums-Written By FaizaFoxy
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Siasa yamtia Akili Baby Madaha..Amekata Shauri Kuachana na Skendo na Utoto ili.........


Baby Madaha Katika Pozi
BAADA ya kushuhudia wasanii wenzake wakijiingiza katika siasa na kuanguka, staa wa muziki na filamu, Baby Madaha ametia akili na kusema sasa atatulia kwani ni imani yake siku moja atajiingiza katika jukwaa hilo.

Alisema sasa ameamua kuachana na maisha ya skendo za kila siku kwani aliumizwa sana na madai ya kutumia dawa za kulevya, kitu kilichomuumiza hadi mama yake mzazi.

Ninajiandaa kuwa kiongozi wa kisiasa miaka ijayo, unajua hata wenzetu walioingia kugombea uongozi wa siasa na kushindwa, ilichangiwa na historia ya maisha yao ya kisanii, sisi ni watu wa skendo tu, nimejifunza kitu kutokana na hilo, nimeamua kuacha utoto, sitaki tena skendo,” alisema Baby Madaha.
Source:Globalpublishers
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Updates: Mkutano wa Edward Lowassa na wanawake wa DSM kutoka Ukumbi wa Millenium Tower


Kama tulivyowatangazia jana rais matarajiwa wa awamu ya tano Kamanda mpambanaji asiyechoka na mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa atalihutubia Taifa kupitia wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kusikiliza kilio cha wanawake wa Tanzania na atatoa mwelekeo wa UKAWA kwa wanawake na Taifa kwa ujumla baada ya kushika dola mwezi Oktoba.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi saa 8 mchana na utarushwa moja kwa moja na kituo bora cha Televsheni Tanzania cha ITV.

Kati ya wanaotarajiwa kuhudhuria ni wanawake wajasiriamali,mama ntilie,wafanya usafi,akina mama wa nyumbani,wanaoishi katika mazingira magumu,wenye ulemavu na waliojariwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Mgombea huyo wa Urais kupitia UKAWA atakutana na wanawake hao ikiwa ni siku moja tangu serikali ya CCM kumpiga marufuku kukutana na wafanyabiahsra mbalimbali masokoni,wagonjwa mahospitalini na pia kumzuia kupanda daladala.

Wakati Lowassa akitendewa hayo mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu amekuwa akisindikizwa na polisi kutembelea wagonjwa mahospitalini na ni juzi tu alikuwa katika hospitali ya HUruma Mkuu Rombo ambapo alikutana na wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo na kusababisha shughuli katika hospitali hiyo kusimama kwa zaidi ya saa tatu.

Timu ya wanahabari wa UKAWA imeshafika hapa Ukumbini na tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri kabla na wakati wa mkutano.

Karibuni..
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

UKAWA Mnaniharibia Mwanangu, Nakosa Raha Nyumbani Kwangu Mwenyewe


Kila nikitaka kwenda nyumbani kwangu,nasitasita. Natafakari namna na kujibu mapigo ya mpigo toka kwa mwanangu. Kijana wangu huyu aliye Chuo Kikuu,akiwa likizoni sasa,ananitambia na kunibeza katika nyumba yangu mwenyewe.

Najuta kumpa uhuru wa kidemokrasia tangu akiwa Shule ya Msingi. Kila akiniona ananitambia kuhusu UKAWA na kukwama kwetu kama CCM.

Nimejaribu kumwambia kuwa mimi sipo tena kwenye kampeni za CCM. Bado ananing'ang'ania. Ananibakisha CCM na kunihusisha moja kwa moja na kampeni za wagombea wetu kuanzia Dr.Magufuli, Mama Samia, wale wa Ubunge na Udiwani.

Nyumba yangu mwenyewe imegeuka uwanja wa tambo na vikumbo vya kikampeni. Yeye amejipambanua kuwa ni mfuasi wa UKAWA kupitia CHADEMA.

Leo, ameshanipigia simu kujiproud kuwa Lowassa anaibomoa ngome ya CCM pale Millenium Towers. Anadai kuwa Lowassa atawateka wanawake wa Tanzania na kuifanya CCM ibaki na wazee tu kama wapigakura wake.

Akajinasibu kuwa wanawake wa Tanzania wanaiacha mkono CCM na inaelekea kuyumba pamoja ya karata yake ya kumsimamisha Mama Samia kama mgombea mwenza.

Leo pia, amenidokeza kuwa watanzania hawa si wale. Amesema kuwa ana tafiti zilizo fiti zikionesha kuwa UKAWA ndiyo dawa. Ananisubiri anioneshe nikifika nyumbani jioni.

Lengo lake nalijua. Ni kuninyanyasa kisiasa lakini kisasa. Kwa hoja za haja bila kubadili lahaja. Najiandaa,kwa kujisomea nyaraka za haraka na baraka,kwenda kupindua tafiti zake. Nikifika nyumbani, kampeni za chumba kwa chumba zitaanza.

UKAWA mmeniharibia mwanangu. Kwasasa hadi ana kibwagizo chake: MAGUFULI APIGE KAMPENI, LOWASSA ATAPIGIWA KURA! Kazi kwelikweli.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

UKAWA Kutumia Viwanja wa Jangwani Jumamosi


Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene imesema kuwa

Ghafla hiyo itafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa malalamiko yao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Tazama Picha za Mafuriko ya Wanawake Waliojitokeza Millenium Tower Kumsikiliza Lowassa, Wengi Wamekosa Nafasi na Kubakia Nje




Ni mkutano wa wanawake wa ukawa na mh lowasa hapa jengo la millenium TOWER Dar es salaam,hizi ni picha za awali,hizi ni picha za awali ambazo nimekuwekea hapa kutoka katika mkutano huo.LOWASA bado hajawasili hapa ila idadi ya wanawake waliojitokeza hapa ni wengi sana kiasi cha kutokutosha katika jengo hili na sasa watu wanasubiri hatma yao kama watahamisha mkutano au italazimu wengine kuwa wapole na kusubiri nje kidogo.
Picha kamili za tukio hili zitakujia baadae kadiri muda unavyozidi kwenda msomaji wetu




























TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

James Lembeli Aitaka Ikulu Imsafishe Pia Lowassa Kama Ilivyowasafishwa Watuhumiwa Wa Escrow


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge kuchunguza madhara ya Operesheni Tokomeza, James Lembeli, amekosoa ‘mchezo mchafu’ wa serikali kuwasafisha baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali.

Amehoji kama suala ni kusafishana, kwanini juhudi kama hizo zisitumike kuwasafisha wengine pia kama Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.

Lowassa alijiuzulu wadhifa wake kutokana na sakata la mtambo wa kufua umeme wa kampuni ya Richmond, mwaka 2007.

Wengine waliojiuzulu kufuatia sakata hilo ni Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao wote walikuwa mawaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati sakata hilo lilipoibuka bungeni mwaka 2008.

Akichangia hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2015/16 bungeni jana, Lembeli alisema, tabia hiyo italeta giza. Alisisitiza tabia ya kuwasafisha viongozi wachache na kuwaacha wengine ni mbaya.

“Kama kusafishana basi tusafishane wote na siyo watu wachache tu. 
 
“Nchi hii sasa inaenda kubaya, watu wanawekwa kwenye makundi…kama kusafishana tusafishane wote na kama siyo hivyo huko tunakoenda kuna giza. Tabia iliyozuka sasa ya kusafishana na kuwaacha wengine ni mbaya,” alisema Lembeli ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.

Alisema licha ya kuwa alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond lililomlazimisha Lowasa ajiuzulu, kwa sasa haoni sababu za kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Monduli naye kutosafishwa.

Tokomeza
Alisema ripoti ya kamati yake ya Tokomeza, haikuwatia hatiani waliokuwa mawaziri watatu, Dk. Emmanuel Nchimbi-Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki-Maliasili na Utalii na Shamsi Vuai Nahodha- Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, isipokuwa waziri mmoja, Dk. Mathayo David Mathayo-Mifugo na Uvuvi.

“Nimeshtuka kusikia ripoti ya Tume ya Kimahakama ya Uchunguzi kuhusu sakata la Operesheni Tokomeza imesema mawaziri hao hawana makosa…kamati yangu iliweka bayana kwamba hao hawakuwa na makosa, kuna siri gani hapo,” alihoji na kuongeza:

“Lakini ripoti hiyo haizungumzii namna ya kuwalipa fidia ndugu wa watu waliokufa, waliojeruhiwa na kupata ulemavu au kuharibiwa mali zao.”

Alimtaja pia Ezekiel Maige, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, kwamba naye pia anahangaika na anastahili kusafishwa.

Tegeta  Escrow
Kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, alisema, matokeo ya uchunguzi uliofanywa na serikali umewasafisha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi na kuwaacha wengine.

Alisema tatizo kubwa la sakata la Akaunti ya Escrow ni wale walioidhinisha fedha hizo kutolewa na siyo waliwekewa fedha kwenye akaunti zao. Kiasi cha Sh. bilioni 301 zilichotwa katika akaunti hiyo.

Alisema wakati akina Prof. Muhongo na Maswi wanasafishwa, akina Prof. Anna Tibaijuka wanahangaika kwa kutiwa hatiani na sakata hilo.

Alisema wakati Prof. Tibaijuka anahangaika kutokana na kuwekewa fedha kwenye akaunti yake, waliohusika kuidhinisha fedha hizo kutoka hawajachukuliwa hatua yo yote.
 
Alidai Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, naye anahangaika kwa kuwekewa fedha hizo, lakini kwa mujibu wa maelezo yake fedha hizo ni malipo ya kazi aliyokuwa ameifanya ya kutoa ushauri ambayo ni haki yake.

Ezekiel Wenje
Kwa upande wake, Mbunge wa Nyamagana, Ezakia Wenje, (Chadema), alirusha kijembe kwa watuhumiwa wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, akisema haiwezekani kwa mtu ambaye yumo kwenye ‘dili’ la kashfa za fedha asafishwe.

“Kosa la escrow ni wale walioidhinisha fedha hizo zitoke. Nikisikia mbunge yumo katika kila dili halafu anajisifia nje kuwa yeye ni ‘nyoka wa makengeza’ huyo huwezi kumsafisha,” alisema.

 Sugu
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, amehoji sababu za serikali kununua magari 700 ya deraya na ya maji ya kuwasha badala ya kuipa fedha Tume ya Uchaguzi (NEC) isajili wapiga kura.

NEC iko taabani kifedha na imeshindwa kusajili wapiga kura na kununua vifaa vya kusajili kielektroniki (BVR).  

Akiongea kwa mbwembwe na vibwagizo wakati wa kuchangia hotuba hiyo, Mbilinyi alisema inashangaza kuona kuwa hakuna kipaumbele. Alisema kati ya deraya (magari yasiyopenya risasi) 700 yanayonunuliwa  anaomba 500 yapelekwe Mbeya ili wayafanyie kazi.

Sugu alisema wapinzani hawana ugomvi na serikali lakini wanachozungumzia ni masuala ya kutetea umma.

Alitoa mfano wa kura ya maoni wapinzani walisema haitafanyika, lakini serikali ikang’ang’ania kuwa itapigwa Aprili 30 jambo ambalo halikufanyika.

Aliongeza kuwa kuna msemo kuwa namba hazidanganyi, lakini watu huongopa hivyo serikali ya CCM ikubali kuwa hakuna sababu ya kuwadanganya wananchi kwa vile ukweli unaonekana.

“Wanawake  au wanaume wanadanganya, lakini namba haziongopi 2+2 ni sawasawa na 4,” alisema Sugu na kutamba kuwa atashinda uchaguzi wa Oktoba.

Akizungumza kwa kuweka lugha za kimziki kama ‘yaah men’‘kamooni’ aliitaka CCM na serikali wasipate hofu (kupaniki) bali wawasikilize na wapinzani kwa vile nia ni kupeleka mbele maslahi ya nchi. 
 
Mbunge mmoja alikifananisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ng’ombe anayesubiri kuchinjwa.

CCM inaelekea kibla kama ng’ombe anayesubiri kisu, tumechoka tunataka kunufaika na rasilimali zetu. Ikifika Oktoba tunaichinja,”alisema Kuluthum Mchuchuri  (CUF Viti Maalum).

Alisema Watanzania wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu na si sera, bajeti  wala mipango ya CCM.

Akitaja baadhi ya mambo yanayoipeleka CCM kibla ni pamoja kujenga maabara wakati hakuna walimu wa sayansi.
 
Alisema shule kama Mwara, Mwaseni na Umwe mkoani humo hazina walimu lakini maabara zinashinikizwa kujengwa.
 
Lakini pia vijembe viliendelea  pale Zarina Madabida (Viti Maalum CCM), alipowafananisha wapinzani na wake wenza wa CCM, akisema hawawezi kuisifia CCM kwani kufanya hivyo ni sawa na mke mwenza kumsifia mwenzake.
 
Mbunge wa NCCR-Mageuzi Kasulu Mjini, Mosses Machali, alipinga kuwa serikali ya CCM haiwezi kujenga maabara bali ni wananchi ambao wanachangishwa fedha na wanashiriki kujenga majengo hayo.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, aliulipua ujenzi wa barabara ziendazo haraka jijini Dar es Salaam (Dart) kuwa ni chanzo cha mafuriko. 
 
Alisema barabara hizo zimegeuza Jangwani kuwa uwanja wa mafuriko na kusababisha maji kujaa juu ya barabara kutokana na ujenzi na vifusi vilivyomwagwa.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, alisema siasa zinazotumia propaganda za udini na ukabila zinatumika kuichafua Chadema.
 
Aliyasema hayo kufuatia maelezo ya Mohamed Amour Chombo (CCM) Magomeni, aliyesema Ukawa wanashangaza kudai wataondoa ubaguzi wakati ndiyo vinara wa kubagua.

Chombo alieleza kuwa Cuf ni wabaguzi kwa asilimia 100, akitaja kuwa huko Pemba kiongozi akiomba uongozi hawezi kupewa kama anatokea Unguja. 
 
Na hata Unguja ndicho wanachofanya ni wabaguzi na wanachaguana kwa misingi ya U-Cuf na Upemba.

Aliendelea kusema kuwa, kwa Chadema mtiririko wa uongozi wao unaonyesha jinsi walivyo watu wa eneo moja, baada ya kumaliza maelezo hayo ilifika fursa ya Lema kuchangia na akasema Chombo anastahili kupigwa risasi.

Akimshambulia zaidi, alisema ingekuwa ni Korea Kaskazini mbunge kama huyo Waziri wa Ulinzi, angeamuru apigwe risasi.

Alionya kuwa kuendelea kuendesha nchi kwa utaratibu wa udini na ukabila kutasababisha taifa kuparaganyika.

Waziri wa zamani wa elimu, Prof. Athumani Kapuya, ametahadharisha kuwa sera ya elimu inayoelekeza Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia taasisi zote za elimu itahatarisha amani ya taifa.
 
Alisema sera ya elimu itateketeza amani ya Tanzania  na kwamba yanahitajika  mapinduzi ya elimu.

Sababu Zilizosaidia Ndege ya Nkurunzinza Isitunguliwe Bujumbura


Pierre Nkurunzinza janja janja sana huyu bwana,hata jana nchini mwake hakuondoka na ndege ya nchi yake...ili kuwapoteza maboya maadui wake alikodi ndege toka South Africa ikaja kumchukua Bujumbura - Dar es Salaam.Hata "Call Sign" yake haikuwa inaita kama "Burundi 001" ilikuwa inaita kwa Registration number yake ambayo ni ya South Africa,maana nasikia alipanda LearJet45(LJ45) yenye usajili wa ZS-OPR ambayo ni usajili wa Afrika Kusini

Sasa kama Rais alifikia kukodi ndege toka Afrika Kusini maanake alianza kunusa harufu za uasi toka kwa watu wake,ambao pengine angekuja na ndege ya Serikali kwayo Marubani wake ni Wanajeshi wangeweza kumuhujumu kwa namna yoyote ile.Hii kukodi ndege ya nchi nyingine na kuendeshwa na marubani ambao ni raia wa nchi nyingine ya Afrika kusini ndio imemuokoa jana Rais Pierre Nkurunzinza,laa sivyo kama angekuwa amekuja na ndege ya Serikali ya Burundi basi historia ya mwaka 1994 ingejirudia jana ktk uwanja wa ndege wa Bujumbura kwa Nkurunzinza kuripuliwa na ndio ingekuwa mwanzo wa machafuko kati ya wale wanaomuungu Nkurunzinza na wale wasio watiifu kwake


Kwenye usafiri wa anga kuna kitu wanaita "Call Sign",huu huwa ni muito wa ndege au utambulisho wake inapokuwa ktk safari zake,utambulisho huu unaweza kuwa ni namba ya usajili ya ndege,au jina la kampuni ya ndege au jina "mahalia" linaloambatana na "flight number"...kwa mfano wa jina "mahalia" kwa ndege za shirika la umma la Afrika Kusini ni "springbok",huyu ni mnyama mwenye sifa na heshima kwa S.Africa,British Airway wao ni "Speedbird",wakati mashirika kama Fly 540 hujiita kama "swift Tango" n.k

Kwa mfano Tanzania shirika la ndege la fast jet "call sign" yake hujiita kama "Greybird" kutokana na picha ya ndege wa kijivu kama alama ya ndege pale mkiani mwa ndege zao.Kwa hiyo hata watu mashuhuri duniani huwa na "call sign" zao wawapo angani au ardhini iwe tu ni ndani ya ndege,mfano Rais wa Marekani akiwa ndani ya ndege ya Rais "call sign" yake huwa ni "Air Force One", akiwa ndani ya meli ataitwa kama "Marine One";kwetu hapa Tanzania ndege ikiwa imebeba rais hujitambulisha kama "Tanzania One",akiwa makamu wa Rais "Tanzania Two" na akiwa Waziri mkuu rubani huita "Tanzania Three".

Tukirudi kwenye mada ya Nkurunzinza Pierre,jana wakati akiondoka Bujumbura kuja Tanzania hakujitambulisha kama "Burundi One" bali marubani wa kukodiwa toka Afrika Kusini waliita kwa "Call sign" ya "ZS-OPR",kitu ambacho kilifanywa kuwa siri ya nani alikuwa ndani ya ndege hiyo,kwa aina ya usajili wa ndege maadui wa Nkurunzinza iliwawia vigumu kujua hasa ni nani yupo ndani ya ndege hiyo na wasingefanya lolote sababu usajili wa ndege ilikuwa ni Afrika Kusini.

Mara baada ya mkutano hapa DSM,Nkurunzinza alitaka kurudi kwa lazima Bujumbura ili akahutubie Taifa kupitia Radio na Tv za Serikali,kujiamini kwako kulikuwa na sababu ya aina ya ndege aliyotumia ili kutua ktk uwanja wa Bujumbura,kitu ambacho aliamini maadui zake hawawezi "kuitungua" kwa sababu zifuatazo:

(1)Ilikuwa ni ndege ya kiraia toka Afrika Kusini

(2)Ilikuwa ndege inayoongozwa na marubani raia wa S.Afrika.

Kuitungua ndege hii yenye marubani wa Afrika Kusini tena "raia" waliombeba "mteja" aliyeikodi,ingeamsha mgogoro mpya wa kidiplomasia ambao "maadui" zake wasingeweza kukubali mtego huo

Nkurunzinza aliondoka Dar es Salaam milango ya saa 1815hrs,lakini baada ya kama saa moja na nusu alirudi tena kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dsm,hii ni baada ya kujaribu kutua mara mbili katika uwanja wa Bujumbura kwa "Call sign" ya " ZS-OPR" badala ya "Burundi One".Hata baada ya rubani kuulizwa mara kadhaa "status of souls on board" alisisitiza kuwa ni "customers" waliomkodi toka Bujumbura-Dsm-Bujumbura.

Baadae Rubani wa ndege akaambiwa "Clear to land at your own risk"...hii ni baada ya chumba cha waongoza ndege kuwa tayari mikononi mwa wanajeshi wasio watiifu kwa Nkurunzinza,hali hii ilimfanya Rubani kugeuza na ku-opt Entebbe International Airport,ambapo Mseven hakuwa tayari,ndipo Pierre akaamua kurudi kwa "Baba" zake Tanzania,mpaka sasa hajulikani amefikia sehemu gani ktk jiji la Dsm,hata Waziri Membe alipooulizwa leo kuwa Nkurunzinza yupo Tz sehemu gani,hakutaka kusema mahali alipo

Hiki ndio kitu pekee kilichomuokoa Brother Nkurunzinza,vinginevyo maadau zake waliokuwa wamefunga mipaka na kutawala viwanja vya ndege wangefanya lolote endapo tu ndege aliyokuwa anatumia ingekuwa ni ile ya Rais ambayo huitumia mara kwa mara,maana kwa maadaui zake kurudi kwa Nkurunzinza toka Dsm na kuhutubia Taifa ingekuwa ni pigo kwani ingezuia vuguvugu na harakati za kumuondoa madarakani zilizokwisha anza.

Lakini mbadala mwingine kama Nkurunzinza angekuwa ametumia ndege ya Rais kurudi Bujumbura kwa kulazimisha ni ima maadui zake wangeitungua ndege yake au wangeruhusu itue na kumshikiria Pierre kwa nguvu,lakini kwa sababu ya "mbeleko" ya ndege ya "kiraia" yenye marubani " raia" toka nchi ya Afrika Kusini,Maadui zake walizingatia diplomasia ya kimataifa na kumsihi rubani asitue Bujumbura "if and only among the souls on board,the soul of Nkurunzinza was boarded"...hii ndio ilikuwa nafuu ya Bro Nkurunzinza na "ujanja" wa team yake ya kijasusi,vinginevyo leo tungekuwa tunaongea mengine na pengine kama yale ya mwaka 1994 ambapo baada ya mkutano wa Dsm,watu walipokuwa wanarudi Makwao wakatunguliwa.

Rais Pierre Nkurunziza Arejea Burundi Baada ya Jaribio la Kumpindua..Wanajeshi Watiifu Wadhibiti Maeneo Muhumu


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza  amerejea nchini humo, huku naibu kiongozi wa mapinduzi akikiri kuwa jaribio la kumuangusha Nkurunziza limeshindwa. Umoja wa Mataifa umetaka kurejeshwa haraka utawala wa sheria.

Mshauri mwandamizi wa mawasiliano wa rais Willy Nyamwitwe, alisema Nkurunziza amerejea nchini humo, lakini hakutoa maelezo zaidi kwa kile alichosema ni sababu za kiusalama.

Nkurunziza alikuwa nchi jirani ya Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda siku ya Jumatano wakati mapinduzi yalipotangazwa na Jenerali Godefroid Niyombere, na kufunika wiki kadhaa za maandamano dhidi ya jaribio la rais kutafuta muhula wa tatu.

Taarifa za kurejea kwa rais Nkurunziza hazikuweza kuthibitishwa na duru huru hata hivyo, na uwepo wake umeendelea kuwa kitendawili usiku wa Alhamisi.

Lakini tangazo kwamba amerudi lilifuatia haraka na kukiri kwa naibu kiongozi wa mapinduzi Cyrille Ndayirukiye kwamba mapinduzi hayo yameshindwa.

Ndayikuriye aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kuwa binafsi anatambua kuwa vuguvugu lao limeshindwa.

Wanajeshi Watiifu wadhibiti vituo muhimu
Mapema Alhamis, wanajeshi watiifu kwa rais walisema walizuwia mashambulizi mawili makubwa yaliyofanywa na wapinzani katika mapambano makali ya kudhibiti kituo chenye umuhimu wa kimkakati cha redio ya taifa.

Miili ya wanajeshi watatu ilionekana ikiwa imelala mitaani karibu na eneo la mapigano hayo, ishara ya kwanza ya maafa katika kadhia hiyo ya mapinduzi.

Kufikia mchana, mkurugenzi wa kituo hicho Jerome Nkokirantevye alisema wanajeshi watiifu ndiyo walikuwa wanakidhibiti kituo hicho.

Afisa mwanadamizi wa polisi alithibitisha taarifa hizo na kusema jana jioni kuwa wanajeshi wanaounga mkono mapinduzi walisambaratika baada ya mashambulizi yao dhidi ya Televisheni ya taifa RTNB na jengo la redio katika mji mkuu kukandamizwa. Alisema baadhi ya waasi tayari wamejisalimisha na wengine walikimbia.

Tangazo la mapinduzi la Jumatano lilisababisha ukosoaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na kuibua hofu ya kurejea katika vurugu kubwa katika taifa hilo maskini, ambalo bado linaendelea kuhisi athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 vilivyomalizika mwaka 2006, na kugharimu maisha ya maelfu ya Warundi.

Baraza la Usalama laonya
Marekani ilisisitiza Alhamis kuwa Nkurunziza ndiye rais halali wa Burundi . Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana katika kikao cha dharura siku ya Alhamis, lililaani jaribio hilo la mapinduzi, na kutaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria na kufanyika kwa uchaguzi kwa kuzingatia makubaliano ya Arusha.

Katika taarifa iliyosomwa na Raimonda Murmokaite, balozi wa Lithuania katika Umoja wa Umoja wa Mataifa, na rais wa barala hilo kwa mwezi wa Mei, baraza hilo lenye wanachama 15 lilieza utayarifu wake kuchukulia hatua vitendo vya vurugu nchini Burundi vinavyotishia amani na usalama.

"Wanachama wa baraza la usalama wamelaani machafuko nchini Burundi na hasa wamewalaani wanaochochea vurugu za aina yoyote dhidi ya raia, na wale wanaotaka kutwaa madaraka kwa njia zisizohalali," alisema Murmokaite.

"Wanachama wa baraza la usalama wametoa wito kwa pande zote kutotumia vurugu na kutoa kipaumbele kwa amani na usalama. Baraza pia limerejelea uungaji wake mkono wa juhudi la mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Said Djinnit, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki."

Chanzo: DW

Ikulu: Nkurunziza Hayupo Tanzania, Alishaondoka, Tanzania haina cha kusema juu ya alipo Nkurunziza.


Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Habari Ikulu,Salva Rweyemamu amenukuliwa na Redio BBC Swahili akisema kuwa Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza hayupo Tanzania. Akizungumza na BBC Swahili, Rweyemamu amesema kuwa Nkurunziza alishaondoka Tanzania na hivyo Tanzania haina cha kusema juu ya alipo Nkurunziza.

The saga continues!

Msemaji wa Nkurunziza amethibitisha kuwa Nkurunziza ameondoka Tanzania. Lakini,amekataa kusema alipo kwa sababu za kiusalama. Msemaji huyo amedai kuwa Rais Nkurunziza bado anadhibiti utawala wa Burundi

Serukamba Awasha "MOTO" Bungeni Kuhusu Sakata la Escrow na Opareshi Tokomeza.......Ashangazwa Na Kitendo Cha Ikulu Kuwasafisha Baadhi Ya Watuhumiwa


MBUNGE wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), ametonesha vidonda vya ufisadi baada ya kuzungumzia ripoti ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue iliyowasafisha baadhi ya watendaji serikalini waliohusika katika kashfa ya Escrow.


Serukamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, alishangazwa na taarifa hiyo kuwasafisha baadhi ya watu waliohusishwa katika kashfa hiyo na kuwaacha wengine, jambo ambalo alisema ni ubaguzi.

Kauli hiyo aliitoa  bungeni mjini Dodoma jana alipokuwa akichangia Hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoiwasilisha bungeni juzi akiomba  Sh trilioni 5 kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Katika mchango wake, Serukamba alisema ni vizuri Bunge likaitaka Serikali itangaze kuwa wote waliohusishwa katika kashfa hiyo nao ni wasafi.

Alisema haoni mantiki kwa Serikali kumsafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Maswi na Waziri  Profesa Sospeter Muhongo na kuwaacha wengine waliowajibika pamoja.

Serukamba alisema kwa kuwa Serikali imewasafisha viongozi hao ni wazi kuwa muamala uliofanyika wa uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow ni halali.

Mbunge huyo alisema ili kutenda haki kwa watu wote ni vema wanasiasa wengine waliojiuzulu nyadhifa zao na kuwajibishwa kwa Azimio la Bunge warejeshwe katika nyadhifa zao.

Waliopoteza nyadhifa zao kutokana na kashfa ya Escrow ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, William Ngeleja.

“Kuhusu suala la Escrow, juzi Katibu Mkuu Kiongozi alitoa ripoti baada ya uchunguzi kufanyika ripoti ikasema katibu mkuu wake na waziri wake ni safi maana yake mwamala ule ni safi.

“Kama mwamala ule ni safi, katibu ni safi waziri ni safi, Chenge anakuwaje mchafu? Tibaijuka anakuwaje mchafu? Ngeleja anakuwaje mchafu?  Mliowapeleka mahakamani wanakuwaje wachafu?  Haiwezekani tuache hizi ni style za zamani.

“Bunge lako linadhalilishwa watu walidanganya watu walileta document (nyaraka) feki wanatetewa, Tibaijuka tulimhukumu kwa nini?  Ina maana kwa Serikali hii kuna watu ni wazuri na wengine ni wabaya tuambieni. Nataka waziri mkuu aje atuambie usafi wa hawa watu ni nini.

“Jingine mheshimiwa spika ni suala la Tokomeza, mmefanya vizuri sana, mheshimiwa spika tuliomba ripoti ya Tokomeza hawakuleta na kama Serikali mmesema mawaziri wale ni safi naomba muwarudishe katika wizara zao.

“Kule Kenya kipindi fulani Waziri wa Fedha alituhumiwa kwamba amekula rushwa akajiuzulu, Mwai Kibaki (rais mstaafu) akaunda tume ya judicial (tume ya kimahakama) kama mlivyounda kwenye Tokomeza, ripoti ilipotoka ilionyesha kuwa Waziri wa Fedha, Amos Kimunya hana kosa lolote, rais alimteua kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

“Mnapoamua kuchukua hizi njia za juu za good governance (utawala bora) msiishie nusu, haiwezekani muishie kwenye nusu, tukiamua kuchunguza na tukabaini kuwa hawakukosea tunawarudisha kwenye nafasi zao, ndiyo matakwa ya good governance (utawala bora). Tuache usanii hapa kwenye hili jambo.

“Kuna watu hapa Maige alituhumiwa kuwa alisafirisha wale wanyama twiga kwenda nje, muundieni tume ili  tuone kweli kama ni yeye ndiye alikwenda kwenye ndege kuwaingiza pundamilia ili na yeye mumsafishe mbona mnasafisha watu nusu, hii ni nini?

“Akina Ngeleja hapa akina Mkulo waundieni tume wote tujue kama walikosea. Haiwezekani muumize wachache mimi katika hili hapana kama kuna jambo linaniumiza ni injustice, haiwezikani tuwe na Serikali ya double standard (ndumilakuwili).

“Walijiuzulu akina Karamagi (aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini) hapa akina Msabaha (aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki), waziri mkuu (Edward Lowassa). Kwa nini hamkuunda judicial inquiry (tume)?” alisema na kuhoji Serukamba.

Mbunge huyo alisema inaweza kuwa ndiyo njia nzuri za utawala bora kwa mtu aliyejiuzulu kuundiwa tume  kujua kama kweli alikosea arudishwe katika nafasi yake.

“Suala hili la Escrow mheshimiwa spika lazima akina Chenge nao wasafishwe, vinginevyo mniambie na hawa mliowasafisha ni wachafu. Mnatumia nguvu nyingi kuwasafisha lakini mnafanyaje nusu? Au wengine mna ajenda nao?

“Hebu tuambieni kama kuna ajenda, hapa akina Mwambalaswa walivuliwa uenyekiti wa kamati na wenyewe semeni kwamba hawakukosea kwa nini muishie nusu?

“Hatuwezi kunyamaza tuache uonevu kwa watu haiwezekani, kuna watu ni wema na wengine ni wabaya haiwezekani. Hiki si chama tunachokijua wote. Werema (aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali) aliondoka kwa sababu gani, maana kama mnasema mwamala ni safi waliosimamia wote ni safi wengine ni wachafu.

"Kuna watu Ikulu nao walituhumiwa lakini bado wapo ofisini sasa Werema mlimuondolea nini uanasheria wake?” alisema.

Baada ya kumaliza kuchangia, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) alinyanyuka katika kiti chake na kwenda kumpa mkono Serukamba na baadaye alitoka ndani.

Kwa upande wake Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalasawa (CCM), alipingana na Serukamba katika dhana ya watu kusafishwa.

Mwambalaswa ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo, alisema hapingani na uamuzi wa Bunge.

“Kimsingi mimi sipingani na azimio la Bunge sihitaji kujitetea wala kusafishwa. Mimi nilikuwa mjumbe wa bodi ya Tanesco niliwajibika katika siasa kwa hivyo sihitaji kusafishwa kwa kuwa si mchafu na wala sina matope,” alisema.

Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania


Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.


Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
 
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
 
Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya  ndege.

Kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  BBC  asubuhi  hii  ya  mei  14, Ndege  ya  Rais  huyo  haikuweza  kutua  nchini  Burundi  na  badala  yake  ilirudi  tena  Tanzania  ambapo  mpaka  sasa  Rais  Nkurunzinza  yupo  jijini  Dar  es  Salaam- Tanzania

Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza
Maafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura
Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''
Manuari za kijeshi zingali barabarani mjini Bujumbura

Vijembe Vya Kisiasa Vyatawala Bungeni......Lusinde Asema Dr Slaa Hafai Kuwa Rais Maana Ikulu Sio Wodi Ya Wagonjwa


VIJEMBE vya kisiasa jana vilichukua sehemu kubwa ya mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu unaoendelea, ambapo mvutano mkubwa ulikuwa kati ya Serikali na vyama vya upinzani nani amechoka.

Akizungumza bungeni kwa vijembe, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), alisema hoja ya kambi rasmi ya upinzani kuwa Serikali imechoka, inawezekana ni kweli ila haikuwekwa vizuri.

Alifafanua kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya kukopesha wanafunzi, kutoa huduma ya afya, kujenga barabara kusambaza umeme bila kusahau hata majanga yakitokea, inayofanya kazi ni Serikali na hivyo katika miaka mitano inastahili kuchoka.

Alisema kwa upande wa kambi ya rasmi ya upinzani, hawawezi kuchoka kwa kuwa kazi yao kila mara ni kusema neno lenye tarakimu sita la ‘Hapana’, hata katika masuala ya maendeleo.

Alitoa mfano wa suala la ujenzi wa barabara ya kwenda Jimbo la Hai, ambalo mbunge wake ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), kuwa badala ya kusaidia ujenzi, kazi yao ilikuwa kusema ‘Hapana’.

Alifananisha uchovu wa Serikali na gari la Mbowe alilosema kuwa likitembea kilometa nyingi, siku zote atalipeleka kwa mafundi lipate huduma ya marekebisho na kuendelea na safari, na hivyo hivyo baada ya miaka mitano, kutafanyika uchaguzi na CCM itaendelea kuongoza.

Lusinde aliitaka Kambi Rasmi ya Upinzani, kuzungumzia suala la uchovu kwa nidhamu kwa kuwa ikitafsiriwa vingine itawahusu baadhi ya viongozi wao wanaoendesha vyama hivyo wakati wamechoka.

“Mzee Mtei (Edwin, ambaye ni muasisi wa Chadema) kachoka lakini ndiye anayeongoza chama… Dk Slaa (Willibrod, Katibu Mkuu wa Chadema) naye kachoka mbona mnamtegemea kwa urais huku mkimkataa Profesa (Ibrahim Lipumba)…? Ikulu si wodi ya wagonjwa,” alisema Lusinde.

Lusinde alifananisha Serikali na timu ya mpira iliyoshinda, ambayo alisema lazima ichoke kwa kazi kubwa, tofauti na timu iliyopata sifuri.

Kuhusu madai ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuwa Uchaguzi Mkuu ukisogezwa mbele moto utalipuka, Lusinde alisema Serikali itaweka tarehe yake ya uchaguzi lakini na Mungu pia anayo tarehe yake.

“Hamkumbuki 2005 uchaguzi ulisogezwa mbele baada ya mgombea mwenza wa Chadema kufariki? Ipo tarehe yetu na ya Mungu pia ipo msitishe wananchi,” alisema Lusinde.

Kisa cha Mfalme
Akizungumzia msuguano wa maneno kati ya Kambi Rasmi ya Upinzani na wabunge wa CCM, Lusinde alitoa mfano wa nchi moja ya kifalme, ambayo Mfalme alimuita Waziri Mkuu na Kiongozi wa Upinzani, baada ya kuona wanalumbana sana.

Katika mazungumzo yao, Lusinde alisema Mfalme alimwambia Kiongozi wa Upinzani aombe suala moja apewe na mwenzako atapewa viwili.

Kwa mujibu wa Lusinde, Kiongozi wa Upinzani aliomba wiki nzima ya kutafakari na muda wote badala ya kutafakari anachotaka kupewa na Mfalme, alitafakari kwa nini mwenzake apewe viwili na yeye kimoja.

Baada ya kumalizika kwa wiki hiyo, Kiongozi huyo wa Upinzani kwa mujibu wa Lusinde, alikwenda kwa Mfalme na kumuomba amng’oe jicho ili Waziri Mkuu, ang’olewe macho yote mawili, kwa jinsi mpinzani huyo alivyokuwa na roho mbaya.

Kutokana na kisa hicho, Lusinde aliwasihi Watanzania wasijaribu kuonja sumu katika Uchaguzi Mkuu ujao na kufafanua kuwa mara zote CCM imekuwa ikishindana na wagombea wa vyama Chadema na vingine, lakini leo kuna chama hata hakijasajiliwa kinaitwa ‘ukawa’ (Ukawa, Umoja wa Katiba ya Wananchi).

Naye Mbunge wa Sikonge, Said Mkumba (CCM), alisema ukiona watu wanaungana katika vita, ujue ni dhaifu na hilo ndilo linaloonekana katika Kambi Rasmi ya Upinzani, ambayo inajaribu kuunganisha nguvu ili kushindana na CCM.

Alisema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hauwezi kwenda Ikulu wakati viongozi wake hawajui mafanikio yaliyopatikana tangu Uhuru.

“Huwezi kushinda kwenda Ikulu, bila kushinda katika serikali za mitaa,” alisema na kuongeza kuwa wanasiasa wa upinzani wanatoa kejeli lakini wakikua wataacha hayo maneno.

Mbio za makatibu wakuu: “Mchukue Katibu Mkuu wa Chadema, CUF na CCM wape wakimbie kilometa tano, nani atakuwa amechoka, mnazungumza huku mkijitukana wenyewe,” alisema.

Baada ya tamko hilo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliongeza “Kama mngeendelea kuwepo, tungeanzisha mbio za vigogo tuone nani mchovu.”

Wakijibu hoja hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alisema uchovu unaozungumzwa si wa mwili bali wa akili na wa kufikiri.

Alisema dalili za kuchoka ni hatua ya Taifa katika mwaka mmoja kufanya mambo makubwa kuliko uwezo wake, vikiwemo Uchaguzi Mkuu, Katiba Mpya na utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Conchesta Rwamlaza (Chadema) alisema wakati mwaka uliopita Serikali ilitenga bajeti ya maendeleo Sh bilioni 660, mpaka leo ni bilioni 160 tu zilizotolewa.

“Tukisema Serikali imechoka, usikate tama badala yake ipelekeni ikafanyiwe ‘massage’ ili uchovu utoke,” alisema Rwamlaza.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul, alifafanua kuwa uchovu wa Serikali si sawa na wa afya, kwa kuwa mtu anaweza kukosa afya lakini akawa na busara nzuri au akawa mlemavu lakini ana upeo mzuri.

“Uchovu wa Serikali ni namna inavyokosa vipaumbele na namna mnavyoshindwa kutekeleza mipango. Kwa hiyo wanaosema tufanye riadha hawaelewi kwa nini tunasema Serikali imechoka,” alisema.

Aliwataka wabunge wa CCM wasibeze Ukawa, kwa kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli na wanajua Ukawa ndio suluhisho la matatizo yao.

Dkt. Hamisi Kigwangala acharuka, ataka wagombea urais wanaotumia fedha majina yao yakatwe


MBUNGE wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Dkt. Khamis Kigwangala amekitahadharisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kihakikishe hakiteui mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu atakayebainika kuusaka uongozi kwa kutumia fedha vinginevyo kitaanguka vibaya kwenye uchaguzi huo.

Dkt. Kigwangala ambaye ni mmoja wa wana CCM walioonesha nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM alitoa tahadhari hiyo alipokuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Nzega na vitongoji vyake katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Parking mjini humo.


Alisema wakati Taifa likijipanga kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ni muhimu kwa CCM ikajipanga vizuri katika kupanga safu ya wagombea wake kuanzia ngazi zote za udiwani, ubunge na urais kwa kuhakikisha haisimamishi wale wote walioanza kusaka uongozi huo kwa kutumia fedha.

Alisema baadhi ya walioonesha nia ya kutaka kuteuliwa kugombea nafasi ya urais hivi sasa wanapitapita maeneo mbalimbali wakigawa fedha kwa wajumbe watakaohusika na vikao vya uteuzi ili waweze kuteuliwa hali ambayo alisema inapingana na tararibu na kanuni za CCM.

“Ndugu zangu binafsi naendelea kuwathibitishia kwamba nia yangu ya kutaka kugombea urais wa nchi ipo pale pale, na niwaeleze wazi kwamba sijatoa uamuzi kuhusu kugombea kwangu tena ubunge katika jimbo hili la Nzega, kwanza nimejikita kwenye urais, iwapo nitashindwa huko ndipo nitatoa uamuzi kama nitagombea ubunge au laa,”

“Hata hivyo napenda nitumie nafasi hii kukitahadharisha Chama changu cha CCM kiwe makini katika uteuzi wa mgombea wake katika nafasi hii nyeti ya urais wa Jamhuri ya Muungano, isifanye kosa hata kidogo kwa kumteua mtu ye yote ambaye tayari ameonesha dhahiri kuusaka urais kwa kutumia fedha,”

“Tunataka CCM isimamishe mgombea aliye safi asiye na doa lolote au kashifa yoyote ya ufisadi katika nchi hii, bali izingatie mtu mwenye agenda na anayeeleza iwapo atachaguliwa kuwa rais atawatendea kitu gani watanzania, siyo sifa ya kuwa na fedha nyingi, nyingine tunajua zimeibwa kutoka serikalini, hii hatukubali,” alieleza Dkt. Kigwangala.

Alisema yeye binafsi anaamini CCM itahakikisha hakuna mgombea ye yote ambaye amebainika tayari anakwenda kinyume cha kanuni na maadili ya chama na ambao hivi sasa wanapitapita kwa wajumbe wa vikao vya uteuzi wakimwaga fedha atakayeteuliwa bali majina yao yote yatakatwa mapema.

Akifafanua Dkt. Kigwangala alisema iwapo CCM itamsimamisha mgombea ye yote mwenye dosari na aliyebainika kutumia fedha katika kuusaka uongozi ni wazi watanzania watahoji maana wengi sasa ni wajanja na wana akili, ni vigezo vipi vilivyotumika kumteua maana CCM daima inaimba rushwa ni adui wa haki, sasa lazima ioneshe kwa vitendo jinsi inavyoichukia rushwa.

“Hawa wanaotumia fedha mpaka hivi sasa hawajaweza kuwaeleza wananchi iwapo watachaguliwa watawafanyia nini, binafsi mimi nina agenda na hoja ya kwa nini nataka kugombea urais, na nimeandikika kitabu kueleza nitakayoyafanya, naamini wengine walioonesha nia ni dhaifu sana, hawana agenda yoyote ya maana mbali ya kuegemea kwenye uwezo wao wa kifedha,”

“Hata chama changu cha CCM hakiamini katika watu wanaotumia fedha, kanuni zetu zikiheshimiwa katika vikao vya awali, majina ya wengi wao yatakatwa hata kabla ya kufikishwa kwenye vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri kuu ya Taifa (NEC), na wengi mtashangaa maana majina yatakayojitokeza ni ya wagombea vijana,” alieleza Dkt. Kigwangala.

Aidha mbunge huyo alisema itakuwa ni ajabu kwa vikao vya uteuzi ndani ya CCM kuteua mgombea ambaye atasababisha wananchi kuwa na maswali mengi juu yake wakati wa kipindi cha kampeni mfano wa wale ambao awali walitakiwa kuvuliwa magamba lakini baadae yaliishia mabegani na wakasafishwa kwa kusamehewa.

“Wapo waliotakiwa kuvuliwa magamba, wanafahamika, leo hii itokee CCM iwasimamishe kama wagombea itakuwa ajabu kubwa, sijui mtu atasimamaje jukwaani kuwanadi, lazima wananchi watahoji hawa wamekuwa wasafi lini? baadhi yao fedha walizonazo walizipata kupitia madaraka waliyokuwa nayo serikalini, leo tena waletwe kwenu eti ndiyo wagombea urais wa CCM, hapana litakuwa ni jambo la kushangaza sana,” alieleza.