Updates: Mkutano wa Edward Lowassa na wanawake wa DSM kutoka Ukumbi wa Millenium Tower


Kama tulivyowatangazia jana rais matarajiwa wa awamu ya tano Kamanda mpambanaji asiyechoka na mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa atalihutubia Taifa kupitia wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kusikiliza kilio cha wanawake wa Tanzania na atatoa mwelekeo wa UKAWA kwa wanawake na Taifa kwa ujumla baada ya kushika dola mwezi Oktoba.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi saa 8 mchana na utarushwa moja kwa moja na kituo bora cha Televsheni Tanzania cha ITV.

Kati ya wanaotarajiwa kuhudhuria ni wanawake wajasiriamali,mama ntilie,wafanya usafi,akina mama wa nyumbani,wanaoishi katika mazingira magumu,wenye ulemavu na waliojariwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Mgombea huyo wa Urais kupitia UKAWA atakutana na wanawake hao ikiwa ni siku moja tangu serikali ya CCM kumpiga marufuku kukutana na wafanyabiahsra mbalimbali masokoni,wagonjwa mahospitalini na pia kumzuia kupanda daladala.

Wakati Lowassa akitendewa hayo mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu amekuwa akisindikizwa na polisi kutembelea wagonjwa mahospitalini na ni juzi tu alikuwa katika hospitali ya HUruma Mkuu Rombo ambapo alikutana na wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo na kusababisha shughuli katika hospitali hiyo kusimama kwa zaidi ya saa tatu.

Timu ya wanahabari wa UKAWA imeshafika hapa Ukumbini na tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri kabla na wakati wa mkutano.

Karibuni..
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI