Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Habari Ikulu,Salva Rweyemamu amenukuliwa na
Redio BBC Swahili akisema kuwa Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza hayupo
Tanzania. Akizungumza na BBC Swahili, Rweyemamu amesema kuwa Nkurunziza
alishaondoka Tanzania na hivyo Tanzania haina cha kusema juu ya alipo
Nkurunziza.
The saga continues!
Msemaji wa Nkurunziza amethibitisha kuwa Nkurunziza ameondoka Tanzania.
Lakini,amekataa kusema alipo kwa sababu za kiusalama. Msemaji huyo
amedai kuwa Rais Nkurunziza bado anadhibiti utawala wa Burundi