Mwigizaji mkongwe wa filamu hapa Bongo, Yvonne Cherly ‘Monalisa’ (33)
amesema kuwa yeye siyo gubegube kwani alishawahi kukaa ndani ya ndoa
lakini sasa ameamua kutulia.
|
Yvonne Cherly ‘Monalisa’ |
Akipiga stori mbili-tatu na Gazeti la Uwazi, Monalisa alisema kuwa hata
kama akiamua kurudi upya kwenye ndoa anaweza na kutilia msisitizo kuwa
mwanaume atayemuoa lazima atambue kuwa anayemuoa ni Yvonne Cherly na si
Monalisa kwani jina hilo litakalokuwepo kwenye cheti cha ndoa.
“Mimi si gubegube, nikiamua kurudi na kufunga ndoa naweza tena nitaolewa
kama Yvonne Cherly kwani ndilo jina langu halisi. Ninachokiwaza kwa
sasa si kukaa ndani ya ndoa bali namna kazi zangu zitakavyoweza
kuonekana zaidi,” alisema Monalisa