Ray C akanusha kuurudia unga, asema watu wanataka kumharibia kwa Jakaya Kikwete

Rehema Chalamila aka Ray C amekanusha taarifa zilizoandikWa na gazeti moja la udaku nchini kuwa ameacha kuendelea na matibabu ya methadone na kurejea kutumia madawa ya kulevya.



Amedai kuwa watu hao wana nia ya kumwaibisha yeye pamoja na Rais Jakaya Kikwete aliyemsaidia. Akizungumza na Bongo5 leo, Ray C amesema hawezi kuacha matibabu au kurudia matumizi ya madawa ya kulevya kwani amebakiza miezi mitano ili kumaliza matibabu hayo.

“Hata unishikie bastola siwezi kurudi kule nilikotoka,” ameiambia Bongo5. “Hakuna mtu anapenda maisha yale, ni matatizo tu ya dunia. Mtu akitoka ametoka, mtu utarudiaje matapishi?” amehoji Ray C ambaye hivi karibuni aliachia wimbo mpya.

“Amini haya magazeti yanatumia majina ya watu kutafuta pesa. Haya magazeti ya Global Publisher yanauza kila siku kwa kumwandika Diamond, yanauza kila siku kwa kumwandika Wema Sepetu. Hizo pesa wanazouza hawatupi hata shilingi. Ni wao tu wanazidi kuwa matajiri. Anajifanya ameokoka, wanajua wananiumiza kiasi gani? Wanajua mheshimiwa itamuumiza kiasi gani? Unaacha mazingira gani? Mheshimiwa akisikia hivyo, daktari gani anaweza kutoa siri za mgonjwa ni daktari yupi? Anataka nigombane na madaktari wangu ambao wananitibu? Huu ni uonevu.”

“Kila siku naenda kula dozi asubuhi na huwezi kukosa hata siku moja na ukikosa siku mbili tu maumivu unayoyapata ni zaidi ya alosto. Nimebakisha kitu kama miezi mitano nimaliz