Wanawake wenye bikra wapo wengi sana zanzibar hata wasomi wa chuo kikuu

Nikiwa katika miaka ya balehe niliwasikia wazee wakijisifu kuwa katika zama zao walikuwa wanaoa wanawake wabichi kabisa yaani bikra. Waliendelea kusema kuwa siku hizi vijana wetu wanakula makapi. Sikuweza kuchangia hoja kwa sababu sikuwa mmoja wao katika mazungumzo yao ila tu nilisikia kwa kuwa nilikuwa pembeni ya nyumba na wao hawakiniona.

Habari ile nilimuuliza kaka ambaye niliweza kumkabili kutokana na ukaribu wake kwangu licha ya kuwa alikwisha oa. Alinifahamisha nini maana ya bikra baada ya kuniuliza swali kuwa nimeshaanza mapenzi au laa. Alinieleza kwa lugha ya staha ambayo sikupata jibu zuri la moja kwa moja. Nilipata ufafanuzi zaidi kijiweni kwa washikaji.

Nilidhamiria nikikua lazima nioe bint bikra na msomi, sikutaka kula makapi ili nami nijinasibu kama wale wazee siku za usoni. Kwa sasa nimemaliza chuo kikuu nina degree, nimeona kabisa ndoto yangu imepotea. Kwa kuwa kaka bado yupo, niliamua kumkata stimu kwa kumkumbusha lile swali la wakati nikiwa balehe. Kaka alicheka sana kisha akajibu kwa mzaha kuwa kama unataka bikra nenda Zanzibar huko ziko nyingi sana wanazitunza hadi waolewe, akaishia hapo bila shaka alihisi kama sikuwa serious.

Wanajamvi naomba mnijuze, je ni kweli kwa yafuatayo:-
1. Je ni kweli Zanzibar kuna bikra za kumwaga?
2. Je wanatumia njia gani hawa kuzitunza bikra hadi umri mkubwa wakati vishawishi na utandawazi ni mkubwa kwa
sasa?
3. Vijana wa kiume wa Zanzibar wanajipoza wapi au nao wana mbinu mbadala ya kukidhi haja zao za mwili?

Nisaidieni ili kama kuna uwezekano niandae nauli na nianze mchakato wa kupata kitambulisho ili niende Zanziba nikaibue bikra ya kuoa