MWILI wa aliyekuwa mwanzilishi wa Kundi la Tip Top
Connection, Abdu Bonge, mapema leo asubuhi ulihamishwa kutoka katika
Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi zaidi.
Mtandao huu ulishuhudia jamaa wa marehemu huyo wakiuhamisha
mwili huo wakisema ni lazima mwili huo ukafanyiwe uchunguzi wa kina
kutokana na utata wa kifo chake.
Mdogo wa marehemu aitwae Idd Taletale alisema endapo
uchunguzi huo utamalizika leo utasafirishwa leo kuelekea Kijiji cha
Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.