Showing posts with label matukio. Show all posts
Showing posts with label matukio. Show all posts

Padri wa Kanisa Katoliki Anaswa Kichakani Ndani Ya Gari Akiwa Na Mrembo UCHI


KAMA mti mbichi unatenda haya, itakuwaje kwa mti mkavu?! Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference, TEC), Padri Anatoly Salawa kufuatia kunaswa kichakani akiwa na mrembo.

Kiongozi huyo wa dini alinaswa hivi karibuni majira ya saa 8: 02 usiku akiwa ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA kwenye kichaka kilichopo maeneo ya viwanda na gereji za magari makubwa, Kurasini jijini Dar.

Huku mvua kubwa ikinyesha na baridi ikipuliza vilivyo achilia mbali baadhi ya maeneo ya jiji kutotulia kwa mafuriko na foleni, waandishi wetu  walipigiwa simu na mlinzi mmoja wa Kimasai wa kwenye gereji hizo na kunyetisha juu ya gari lililosimama karibu na eneo lao la lindo huku likinesanesa.

Mlinzi huyo alieleza kuwa yeye na wenzake walilichunguza kwa makini gari hilo na kuona kuwa ndani yake kulikuwa na watu wawili wa jinsi tofauti lakini walishindwa kujua wazi kilichokuwa kikiendelea.

Mlinzi huyo alisema kuwa mara kwa mara gari kama hilo  limekuwa likifika hapo majira ya usiku wa manane hivyo kuwafanya kuingiwa na shaka.

Waandishi walifika eneo la tukio ndani ya muda mfupi na kuwakuta polisi nao wakiwasili kisha kuchukua kwanza maelezo kwa walinzi hao bila kuwashtua wahusika kwenye gari.

Baada ya mahojiano na walinzi hao, walilifuata gari hilo na kulipekua ambapo hawakuamini macho yao baada ya kumkuta mtu mzima huyo katika gari hilo akiwa na mrembo aliyekuwa mtupu.

Huku mvua ikiendelea kumwagika, padri huyo alionekana akiwa ametaharuki ndani ya gari asijue la kufanya.

Mara baada ya kuwanasa wawili hao, padri alijitetea kwa kusema kuwa, alikuwa ameingiliwa na wahuni katika starehe zake hivyo aliingia kwenye gari na kutimua na mrembo wake.

Jana  padri  huyo  alitafutwa  tena ili kama ana la ziada la kusema alitoe lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na baadaye ikazimwa kabisa.

Baada ya muda simu hiyo iliwashwa tena na ndipo  alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS) . Hata hivyo, SMS hiyo haikujibiwa.


Baada ya SMS hiyo, padri huyo aliendelea kupigiwa simu lakini bado iliita bila kupokelewa ndipo akatumiwa ujumbe mwingine uliosomeka hivi; ‘mkuu tumepata tukio lako ukiwa kichakani ndani ya gari usiku na mrembo akiwa mtupu. Wewe unalizungumziaje tukio hili? Kwa maana nyingine unajiteteaje? Tunaomba maelezo yako’.

Kama ilivyokuwa kwa ujumbe wa kwanza, nao huo haukujibiwa.

Chanzo:  Gazeti  la  Ijumaa/Gpl

Mchungaji Gwajima Avamiwa.....Apigwa Panga Kichwani na Kulazwa ICU


MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima jijini Mwanza, Samson Gwajima na Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Amin Neigwa, wamevamiwa na majambazi ambao wamewajeruhi vibaya kwa kuwakata mapanga vichwani.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Lyila, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.

Akizungumza kwa taabu na mwandishi wetu akiwa wodini kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), alikolazwa kwa matibabu, Neigwa, alisema akiwa sebuleni nyumbani kwake na mkewe, ghafla walimuona msichana wa kazi aliyekuwa nje akichota maji, akiingia ndani kwa kasi na kukimbilia chumbani.

Alisema wakati akitahamaki kilichotokea, watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliingia ndani wakiwa na silaha za jadi kama mapanga, nyundo, vitu vyenye ncha kali na kutaka fedha.

"Walikuwa sita na baadhi yao walifunika sura zao kwa vitambaa, walinitaka niwape pesa...nilipata ujasiri wa kumrukia mmoja wao aliyekuwa na panga na kumkaba ndipo wengine wakanishambulia kwa kutumia silaha zao hadi nikapoteza fahamu," alisema.

Aliongeza kuwa, wakati wanamshambulia wengine walikuwa wanamlazimisha mkewe awape pesa lakini aliwakatalia na baadaye aliamua kuwapa sh. 10,000 ambayo ilikuwepo wakaichukua.

"Kelele nilizopiga wakati tumevamiwa zilisikika kwa majirani ambao walijitokeza ndipo wavamizi wakakimbia," alisema Neigwa ambaye alijeruhiwa kichwani ambapo hadi jana alikuwa akitokwa na damu masikioni.

Baada ya watu hao kukimbia, walienda kuvamia nyumbani kwa Mchungaji Gwajima na kumjeruhi kichwani kwa panga ambapo hivi sasa amelazwa katika hospitali hiyo kwenye Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).

Mchungaji Gwajima ni kaka wa Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, ambaye alivamiwa alipokuwa amelala na familia yake eneo la Lyila na kulazimishwa kutoa fedha.

Akizungumza na mwandishi wetu, Mchungaji wa kanisa hilo, John Kiula,  alisema Mchungaji Gwajima alivamiwa usiku ambapo baadhi ya mashuhuda walidai baadhi ya meno yake yameng'oka.

"Hadi sasa bado hajajitambua, tumetoka kwenye kipimo cha CT-Scan lakini majibu bado hatujapewa tumeambiwa yakiwa
tayari watatujulisha," alisema Mchungaji Kiula.

Mkuu wa Idara ya Dharura hospitalini hapo, Dkt. Derick David, alikiri kuwapokea majeruhi hao usiku na kusema Mchungaji Gwajima alifikishwa akiwa na hali mbaya zaidi kuliko Neigwa.

"Gwajima ana jeraha kubwa kwenye paji la uso ambalo ni kama sentimita mbili hadi tatu kwa urefu kwenda ndani, kipimo cha X-Ray kimeonesha hajapasuka mfupa ila hali yake si nzuri.

"Hadi sasa bado hajitambui, tunatarajia kumfanyia kipimo kikubwa cha CT-Scan ambacho kitaonyesha ameumia kiasi gani lakini Neigwa anaendelea vizuri ingawa naye anahitaji kupimwa na CT-Scan ili kuona majeraha yake kama amepata athari ndani ya kichwa, tunaendelea kuokoa maisha yao," alisema.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo, alikiri kutokea kwa matukio hayo na kuahidi kuyatolea ufafanuzi ambapo baadhi ya watu wamekamatwa wakihusishwa na matukio hayo.

"Mkuu wa Upelelezi Mkoa na timu yake walikuwa wanaendelea na uchunguzi, wakiukamilisha nitalizungumzia kwa undani na kuwataja walioshikiliwa, baadhi ya majambazi hao wametambuliwa na majirani," alisema.

Nyumba ya Diamond Katika Hati Hati..Mafuriko Yaizengea ,Yazungukwa na Mifereji ya Maji ya Mvua


MAFURIKO yanayotokea katika sehemu mbalimbali nchini kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha, yanaizengea nyumba ya nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz iliyopo Tegeta Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar.

Kwa mujibu wa majirani wa staa huyo, nyumba hiyo imejengwa katika njia ya maji (mkondo), jambo ambalo hakulielewa hapo mwanzo, kwani ndiyo sababu kubwa iliyodondosha ukuta wa uzio wake muda mfupi baada ya Diamond kuhamia wiki kadhaa zilizopita.

“Kabla ya ujenzi, kiwanja hiki kilikuwa na njia kuu mbili za maji ambazo wakati wa mvua, zilikuwa zinatiririsha maji kuelekea bondeni, lakini baada ya ujenzi, nguvu ya yale maji yakadondosha ukuta.

“Sasa ukiacha ukuta uliobomoka mwanzoni, kuna njia nyingine ambayo inapitisha maji mengi zaidi ambayo inapita kwenye ukuta wake mwingine na tayari yameanza kuuchimba kwa chini. Mnaweza kuja kuangalia,” alisema jirani mmoja aliyekataa kutaja jina lake.

Waandishi wetu walifika nyumbani hapo na kumkuta fundi ujenzi akijaza kifusi nyuma ya ukuta uliovunjika mwanzo huku upande mwingine wa ukuta  maji yakionekana kutiririka kwa kasi.

Aliyemng’ata na Kumtesa ‘House Girl’ Avamiwa na Majambazi


KESI ya kumtesa mfanyakazi wa ndani inayomkabili mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige (42), imeahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jana kutokana na mshtakiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumkata kwa mapanga.

Shauri hilo litakuja tena Juni 16, mwaka huu endapo hali ya mshtakiwa ikiendelea vizuri.

Mbele ya Hakimu Yohana Yongolo, Wakili upande wa Jamhuri ulidai kwamba shauri hilo lipo mbele ya mahakama hiyo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa ushahidi upande wa mlalamikaji.

Mdhamini wa pili wa mshtakiwa Chausiku Maige, aliiambia mahakama hiyo kwamba Amina ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa alivamiwa na watu wasiojulikana ambapo tukio hilo lilitokea nyumbani kwake Mei 7, mwaka huu.

“Mheshimiwa mtuhumiwa kwa sasa yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Taasisi ya Mifupa (MOI), akiendelea na matibabu baada ya tukio hilo lililotokea nyumbani kwake alfajiri wakati akitoka ndani kuelekea kazini.

“Tulitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Osterbay kisha tulipewa RB/7647/2015. Amina amepata majeraha makubwa sehemu za mkononi pamoja na kichwani,” alidai Chausiku.

Hakimu alimhoji mtuhumiwa huyo kama  eneo analoishi mtuhumiwa huyo ana uhasama na jirani zake, ambapo shahidi huyo alijibu kuwa hajui kwa kuwa haishi naye karibu.

Amina Maige kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo Juni 13, mwaka jana akikabiliwa na tuhuma za kumchoma pasi na kumng’ata mfanyakazi wake wa ndani, Yusta Kashinde (20) hali iliyosababisha maumivu makali mwilini.

Mapinduzi ya Burundi: Rais Pierre Nkurunziza Ahojiwa na Kituo cha habari cha Burundi RTBN.......Asema Yupo Tayari Kumsamehe Mwanajeshi Atakayesalimu Amri


Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.

Katika  mahojiano  hayo  ambayo  Shirika la habari la Reuters lilifanikiwa  kuyanukuu, Rais Nkurunziza amesema  yupo  tayari  kumsamehe  mwanajeshi  yeyote  atakayekubali  kusalimu  amri.

''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi, nawashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.Alinukuliwa akisema.

Muda  mfupi  baada  ya  mahojiano  hayo,  vita kali  ya  majibizano  ya  risasi  iliibuka  karibu na kituo hicho cha habari baina  ya  wanajeshi  watiifu  kwa  rais  huyo  na  wale  waliotangaza  kumpindua.

Hali  hiyo ilikilazimu  kituo  hicho  kuzimwa  na  kisha  kufunguliwa  tena  baada  ya  mapigano  kuisha

Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba wanajipanga kukiteka kituo hicho cha habari cha RTNB  kilicho  chini  ya  udhibiti  wa  wanajeshi  watiifu  kwa  Rais

Huku Mapigano Makali Yakiendelea Huko Burundi, Rais Nkurunzinza Aingia Nchini Humo Kwa Kutumia Helkopta Baada ya Jana Kushindwa

BREAKING NEWZ
Mapigano makali yakivita yanaendelea mjini Bujumbura kati ya wanajeshi. Mapigano hayo yameanza saa tisa alfajiri na tayari zaidi ya watu mia mbili wanahofiwa kupoteza maisha!
........Vile vile inasemekana Nkurunzinza amerejea Burundi kwa usafiri wa helikopta leo alfajiri akitokea DSM, na kushuka ktk kijiji kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi. Haieleweki ameelekea wapi baada ya kutoka ktk kijiji hicho! Ila mashuhuda wamesema msafara wa magari yapatayo kama sita ulikuja kumchukua kutokea katika kijiji hicho!!
.............Source. Reuters& France 24 english - ...................HUYU MTU NI MBISHI SANA I HOPE KUNA VIONGOZI WETU HAPA BONGO WANAOTAKIWA KUJIFUNZA WEWE HAUJAZALIWA NA MADARAKA UMEYAKUTA NA UMEYAPATA KWA SABABU KUNA WALIOKUBALI KUKUACHIA BILA VITA WALA UGOMVI SASA KWA NINI NA WEWE HUTAKI KUACHIA WENGINE KAMA ULIVYOACHIWA? ...MIAKA 10 KWENYE POWER UMESAHAU NINI HASA AMBACHO SASA NDIO UMEKIKUMBUKA BAADA YA MIAKA 10 gademiti ONDOKA BANA WAACHIE NA WENGINE KAMA ULIVYOACHIWA KWA AMANI

Ili Aweze Kuzaa, Wema Sepetu ni Lazima Alale Juu ya Kaburi au Arithiwe na Ndugu Yake Steven Kanumba


Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa ili azae, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya kaburi.

Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.

Akizungumza na waandishi wetu, baba huyo alisema kama kweli Wema alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto) hivyo anatakiwa kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba.

Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).

“Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili, moja ni kufariki dunia au ‘kujikila’ (kujilaani) kwa kutokuzaa, pengine ndicho kilichomtokea Wema,’’ alisema baba Kanumba.

Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo alishafariki dunia kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda kaburini kwake kufanya tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kiasili na mikononi wameshika vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema kukaza moyo.

Alisema kuwa wakiwa kaburini hapo, Wema alitakiwa achotewe mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya kuomba msamaha kwa kilichotokea.

Alisema walitakiwa waende na maziwa, unga wa mtama na hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.

Aliendelea kudadavua kwamba, kwa sasa Kanumba hayupo duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa damu kwenda kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua mlango wa kizazi, hata kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.

Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni bibi yake mzee Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa wanawake walioshindwa kupata watoto au wenye tatizo la kizazi.

Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa, ingekuwa zamani ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa vikali.

Basata Yalaani Tabia Chafu na Isiyo na Maadili Iliyoonyeshwa na Shilole Akiwa Jukwaani Nchini Ubelgiji


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.

Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.

Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.

Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.

Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.

BASATA linapenda kueleza kwamba;

Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua
BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.

Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI

Mgahawa Wauza Nyama ya Binaadamu Nigeria..Wamiliki Wakamatwa


Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.

Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.

Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.

Mwenyekiti wa CCM Marampaka Akutwa na Fuvu la Albino Pamoja na Viungo vya Mikono na Miguu


Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Chigila Gilala mkazi wa kijiji cha Bukigi kata ya Malampaka wilayani Maswa (45) kwa kosa la kukutwa na viungo zinavyodhaniwa kuwa vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa.

Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM katika kijiji hicho na Mganga wa tiba asili alikamatwa nyumbani kwake, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa- alikuwa amewahifadhi majambazi kwa ajili kugangwa (kuzindikwa).

-Akitoa taarifa kwa waandishi wa kamanda wa -jeshi la polisi Mkoani Simiyu Gemini Mushy alieleza kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mwenyekiti huyo lilitokea Mei 9 mwaka huu -majira ya saa 11 jioni katika kijiji hicho.

Kamanda Mushy alisema kuwa askari wakiongozwa na mkuu wa upelelezi katika wilaya ya Maswa walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwepo kwa majambazi nyumbani kwa mganga huyo, kuwa alikuwa amewahifadhi kwa ajili ya kuwazindika.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifanya msako nyumbani kwa mwenyekiti huyo, ambapo- alibainisha kuwa walianza kufanya upekuzi ndani na nje ya nyumba.

“Wakati wakifanya upekuzi huo walikutana na mfuko wa sandarusi ukiwa chini ya lundo la kuni nje ya nyumba- ya mwenyekiti huyo..na katika mfuko huo kulipatikana fuvu la kichwa pamoja na mifupa ya mikono au miguu vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya binadamu” Alisema Mushy.

Kamanda alieleza kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi kama kweli viungo hivyo ni vya binadamu na kama anahusika na uwepo wa viungo hivyo kutokana na -kukutwa nje ya nyumba yake.


Wakati huo huo kamanda Mushy alibainisha kuwa jeshi hilo linamshikilia- Gandula Mashimo mkazi wa kijiji cha Longalombogo kata ya Migato wilaya ya Itilima Mkoani hapa kwa kukutwa na Bunduki ya kivita SMG na risasi 273.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 3:30 usiku kijijini hapo, akiwa embeba siraha hiyo pamoja na risasi katika mfuko wa sandarusi.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani humo, ambapo alikamatwa akiwa njiani kuelekea kusikojulikana.

-
Mushy alieleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini washirika wake, ikiwemo na matumizi ya silaha hiyo, huku akitoa wito kwa wananchi mkoani hapa kutoa taarifa za watu wanaowahisi kuwa siyo wema katika maeneo yao.

Aidha alitoa onyo kwa ambaye anamiliki silaha bila kibali rasmi, kuwa ajisalimishe pamoja na silaha yake mara moja kabla ya msako mkali kuanza.

Aunty Ezekiel Awachafua Mashabiki Wake Kwa Picha Hizi za Kitumbo Wazi


Staa wa bongo movies, Aunt Ezekiel amepondwa na baadhi ya mashabiki wake kwa kupiga picha hizi akionyesha tumbo lake ukigingatia yeye ni mjamzito.

Picha hizi zimekuwa zikisambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii na wengi wameonyesha kuchukizwa na tabia iliyozuka ya mastaa wa Bongo kufanya hivi kwa kuwaiga mastaa wa nchi za ughaibuni.

Wewe je, unamaoni gani juu ya hizi

Wema, Kajala Tena, Wakutana Laivu Club Wakiwa Bwiii..Wakwepeshwa Wasizichape


MAJANGA! Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja na Wema Sepetu ‘Madam’ wametengeneza tena vichwa vya habari baada ya kukutana ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua minong’ono miongoni mwa wadau wengi wa burudani, Risasi Mchanganyiko linakupa hatua kwa hatua.
Msanii wa filamu Bongo,Kajala Masanja akifurahia jambo.
Matukio hayo tofauti kwa wasanii hayo yalitokea ndani na nje ya ukumbi huo katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste  Venus, Lisa Karl Fickenscher  iliyowakutanisha mastaa wengi wa ‘category’ mbalimbali.
SHUNGULI YAANZA VIZURI
Shughuli nzima ilionekana kwenda vizuri, isipokuwa mara chache ambako kulitokea vituo vya hapa na pale, ingawa vingi kati ya hivyo vilisababishwa na baadhi ya wahudhuriaji kuzidiwa na kilevi.
Kajala Masanja akiwa na bandeji kichwani baada ya kupigwa chupa.
WATENGANISHWA
Wakati flani ‘usiku mnene’, Kajala alijongea kwenye jukwaa maalum la waalikwa (V.I.P) kutoka kujichanganya kwa wadau, ambako pia alikuwa amekaa Madam aliyeonekana kuzidiwa na ‘kiburudisho’.
Akitambua wazi kuwa lolote lingeweza kutokea, Petit Man, mtu wa karibu wa Wema, alimshika mkono na kumtoa eneo hilo, lakini muigizaji huyo alipohoji sababu za kuondolewa ‘V.I.P’, aliambiwa kuwa hapakuwa sehemu salama kwa wakati huo. 
Wema Sepetu akiwa kwenye gari.
KAJALA NDANI YA NYUMBA
Kajala alionekana akijiachia kwa mapozi na ‘mihangaiko’ ya hapa na pale ikiwemo kucheza na kubadili vinywaji akiwa sanjari na marafiki zake.Wakati wote, msanii huyo alionekana mwenye furaha iliyoambatana  na tabasamu na vicheko vya mara kwa mara jambo lililotafsiriwa kama tayari alikuwa amepata kiburudisho cha kutosha.
Wema akiongea na mashabiki wake ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar.
AKUTWA NA MKASA
Mapambazuko yalipoanza kulivamia anga, Kajala na ‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.
AMSHIKA MAKALIO
Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo, jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha usoni.
Baada ya tukio hilo, marafiki wa pande zote mbili walijitahidi kutuliza hali ya hewa iliyochafuka na kila mmoja akaendelea na hamsini zake.
Akiwa katika pozi nje ya klabu Maisha.
WEMA SASA
Kwa upande wake, Wema ambaye alipaswa kuwa Msema Chochote (MC) wa hafla hiyo, alipanda jukwaani kwa kusaidiwa na watu kutokana na kuzidiwa na kinywaji kisichojulikana.Baada ya kupanda, muigizaji huyo nyota alishindwa kumudu kuendelea na ratiba, kwani alizungumza maneno yasiyoeleweka na hatimaye kuishia kuwasalimu mashabiki, kitu kilichoharibu shughuli hiyo kwa jumla.
Kajala akiwa Maisha Club kabla ya kujeruhiwa kwa chupa. 
ATOKA UKUMBINI NA GLASI
Baada ya kushuka jukwaani, mmoja wa wapambe wake wa muda mrefu, Petty Man alimshika mkono na kumsindikiza hadi nje, ambako akiwa ameshikilia glasi yake ya kinywaji, Wema aliingia nayo kwenye gari, kabla ya kumwaga kilichokuwemo ndani na kumpa mtu mmoja glasi hiyo ili airudishe ndani.
Wema akiondoka.
Mwandishi wetu alipotaka kujua sababu ya Wema kulewa na kushindwa kufanikisha jambo muhimu, alimtaka kumuacha kwani hakuwa na muda wa mahojiano.“Tafadhali sana (akilitaja jina la mwandishi), sihitaji mahojiano, hapa nimekuja kwenye starehe, naomba uniache,” alisema Wema huku akibamiza mlango wa gari kwa nguvu na kumtaka dereva wake (Petty Man) kuondoa gari.
KUTOKA KWA WADAU
Baadhi ya watu walioshuhudia matukio ya Wema na Kajala kwa nyakati tofauti, walisikika wakisema kuwa ni kama mkosi uliowakumba wawili hao marafiki wa zamani.“Hawa bwana wana matatizo sana, wote wamekutwa na majanga kwenye eneo moja, lakini nadhani hata matatizo yao yanachangiwa sana na bifu lisilokuwa na kichwa wala miguu, wajishushe na wasameheane,” alisikika akisema mdau mmoja.
GPL

Mkenya Aliyehukumiwa Kunyongwa China Kwa Kusafirisha Madawa ya Kulevya


Mwanadada mwenye umri wa miaka 26 huenda akanyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa ya kulevya nchini china ambapo Mkenya huyu Floviance Owino, aliyehudumu kama msaidizi wa nyumbani alitiwa nguvuni May 2013 akisafiri kuelekea Beijing kutokea hapa Nairobi.

Afisi ya ubalozi wa kenya nchini Uchina umethibitisha kwamba huenda Floviance akanyongwa mwaka huu baada ya kifungo chake cha miaka miwili kukamilika na haya maneno ni kwa mujibu wa dada yake ambaye ni Judith Owino. Judith anasema hakufahamu kuwa dada yake alikuwa amesafiri kwenda China hadi alipopata habari kutoka kutoka ubalozi wa kenya nchini humo.


Nilifahamu kwa mara ya kwanza kuwa alikuwa China nilipopata simu kutoka kwa ofisi za ubalozi, nlifahamu pia kwamba yuko kizuizini akisubiri kunyongwa, ofisi ya Mashauri ya nchi za kigeni ilinipa habari kuhusu hukumu ya kunyongwa kwa dada na kunipa kibali cha haraka kusafiri kwenda China’

Serikali ya uchina hata hivyo ilimwarifu Judith kwamba alikuwa na muda mfupi kugeuza hukumu hiyo na kuzuia dada yake asinyongwe, walinishauri nitafute wakili hivyo kwa sasa nahitaji visa kwenda china maana mda unazidi kupotea.

Mpaka sasa Judith hajapata fursa ya kuzungumza na Floviance kwani serikali ya china haikukubali hilo lifanyike  ‘nilitamani sana kuongea nae lakini walinikatalia, Floviane ana mtoto wa miaka minne aliyemuacha Kenya baada ya kusafiri kwenda China’

Je unaweza kununua maisha kwa gharama yoyote?? Nawaomba watanzania wenzangu msifinye biashara haramu ya madawa ya kulevya, mkikamatwa mnaweza kupoteza maisha!

OGM! .....Irene Uwoya Releases Sexy Photos while Taking a Shower in a Bathtub


Through instagram actress Irene Uwoya shared these hot pics of herself being in a bathtub with no piece of cloth to cover her hot chest............

Mkurugenzi Mkuu Vodacom aliyejiuzulu Aula Qatar ......Mitandao Yahusisha Kujiuzulu Kwake na Kashfa ya Upotevu wa Bilioni 700 za Kitanzania


Aliyekuwa  Mkurugenzi  mkuu  wa  Vodacom  aliyejiuzulu hivi  karibuni  Rene Meza amepata shavu katika kampuni nyingine ya mawasiliano  nchini Qatar ijulikayo kama Ooredoo Mynmar kuwa Mwenyekiti  mtendaji  wa tawi la Mynmar.

Aidha, taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana  na kampuni hiyo imesema kwamba Rene Meza atachukua nafasi ya  Ross Cormack ambaye anatarajiwa kuachia nafasi hiyo mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Afrika Kusini umebanisha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom amejiuzulu  ili kufanya kazi nyingine.

Hata hivyo mitandao ya kijamii  mbalimbali  nchini Tanzania imehusisha  kuondoka kwake  na kashfa ya upotevu wa takribani  bilioni 700 fedha za kitanzania ambazo ni sawa dola za Kimarekani  milioni 350.

Taarifa  hizo  zinaarifu  kuwa  bwana Meza alikuwa kwenye  ‘kitimoto’ cha maofisa wa juu wa Kampuni hiyo akihusishwa na kashfa ya kupokea dola milioni 5 kutoka kwa Mmiliki wa Shivacom,Tanil Somaiya ambaye  alimpa  ili  kumziba mdomo   kutokana  na  kashfa   ya  uzalishaji, usambazaji na uuzaji  wa  vocha  bandia  zilizokuwa  zinajulikana  kwa  jina  la  "Jero jero".

Rene Meza alijiunga na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom mwaka 2011 akitokea kampuni ya Bhati Airtel Ltd ya nchini Kenya.

Ifuatayo  ni taarifa iliyotolewa na kampuni ya Ooredoo Mynmar ya nchini Qatar.

Kajala Apigwa Chupa ya Uso Akiwa Club..Mwenyewe Adai Maisha Yanaendelea

STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja, kupitia akaunti yake ya Instagram hivi punde amesema maisha yanaendelea ikiwa ni siku mbili baada ya kupigwa chupa na mtu asiyemfahamu usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa klabu wakati alipokwenda katika shoo ya kumchangia mke wa Mabeste, Maisha Club

Kajala alieleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati akijiandaa kutoka Maisha Club ambapo ghafla akiwa kwenye ngazi alirushiwa chupa kichwani iliyopelekea kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamalia wema waliompeleka Hospitali ya Mwananyamala ambapo alishonwa kwenye jeraha alilolipata.

Staa huyo aliongeza kuwa mtu aliyempiga chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo alikuwa  hamjui na wala hajawahi kumuona mtu huyo.

Picha za Shilole Zazua Gumza Mtandaoni, Mchumba Wake Nuhu Mziwanda Asema Haya Kumtetea

I love you is My Country aka Shilole Kiuno Amejikuta tena leo akiwa Gumzo la watu mitandaoni baada ya picha zenye utata akiwa jukwaaa kuzagaa kwenye mitandao mbali mbali na kujadiliwa hasa Instagram.....

Baada ya Picha hizo Kusambaa Mpenzi wake aliingia mtandaoni na kuposti haya maneno kumtetea:

"Show ni movement na uwezi mkataza mtu kupiga picha ukiwa kwa stage'na kuna nguo za show na nguo za kutoka out kikawaida'ukiruka ruka sana sidiria ni rahisi kuchomoka akina dada mnafaham na mtu yupo stejini anakua hajitambui kama nini kimetokea coz yupo stejin kwenye mood ya kazi na kila mtu ni binadamu na ndio mana wengine wanateleza kwa stage'huyo paparazi aliopiga picha alifanikiwa kuzoom na kipata picha mbaya lakin katika hali ya kawaida na watu waliokua wakicheza nae hawakuweza kugundua lolote'na kiubinaadamu kama muhandishi wa habari hakupaswa kuchagua picha ambayo kaonekana vibaya mana naamini alipata picha nyingi nzuri tu za kupost ila aliamua tu kumchafua'So Mashabiki kumbukeni alikua yupo kazini hakupanga itokee ivyo na yote mradi atoe burudani nzuri kama mlivyomzoea''ambae hana upeo mdogo wa kufikiria ataongea shit ila kaa jiulize ingekutokea wewe ungesemaje?naomba mtusaidie kurepost hii habari'tunawapenda sana"

Haya ni Baadhi ya Maoni ya watu mbali mbali waliokasirishwa na Picha hizo:


MrekebishaTabia
Sitaman hata kuibandika hii picha hapa...kichefuchefu!! hii tabia chafu iliyopitiliza...na si mara yako ya kwanza @shilolekiuno unafanya vituko tadhan mtoto mdogo wkt mtu mzima na watoto wakubwa. Si bahati mbaya amefanya kusudi... mtu mwenyewe kuimba hujui na hata kujiheshimu unashindwa? Kale kaheshima kadogo ulikonako kwa shabiki zako utakapoteza, soon tutasikia umerudi kucheza tamthilia. ....Sijui umekunywa pombe za wapi wewe...!!!

ambassador_angelo

Pole mdada hahaha kazi ndo zilivyobwe kioo cha jamii siku nyingine vaa vizuri sawa mdada mzuri eeeee

mimas_wa_pwiiii

sasa@shiloleliuno kwani hakunaga nguo zenye heshma Dada yangu mbona hiyo nguo IPO wazi kupitiliza ivi mbona wanaume wanavaa vizuri tu kwenye shoo zao why nyie madada hamujiheshimu asee hii sibahti mbaya imekusudiwa nguo yenyewe ni uchi tosha na iyo sidiria ulitegemea Haiti vukaa ebu jiheshimuni bwana munaboaa tuachieni ujinga wenu stejin kwani mukivaa nguo zinazo still hapo kidogo mnakuwa hamujui kuchezaa sheeenzeee zenu wakaa uchi wotee

nyota_ya_warembo

Anamaudhi sana havumiliki kabisa, utavumilia hili baadae anaibuka najingine aisee tutamvumilia mpaka lini!!!!!! Nampenda sana lakini anakero sana, niaibu kusema mbele za watu shilole 'nampenda' watakushangaa

johar_seleman

Afu hapo mbona km kabambiwa ivi mcheki uyo mshua anavomtolea minjicho hahaaaaa ni shigidiiii shidaaa

Siwema Wa Nay Wa Mitego Atiwa Mbaroni.....Kisa Ni Kumpiga Picha Za Uchi Kigogo Wa Serikali


Mzazi mwenzake staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson (27) ametiwa mbaroni na kusota rumande kwa siku kadhaa akidaiwa kujipatia mali kwa njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja serikalini (jina linahifadhiwa kwa sasa).

Mei 2, mwaka huu, Siwema alilala ‘nyuma ya nondo’ (mahabusu) kwa siku mbili katika Kituo Kikuu cha Polisi, Wilaya ya Nyamagana jijini hapa baada ya kukamatwa nyumbani kwake Lumala, Manispaa ya Ilemela.

Kwa mujibu wa chanzo, awali ilidaiwa kuwa, Siwema aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo jijini hapa kwa ahadi ya kufunga naye pingu za maisha kufuatia kigogo huyo kufiwa na mkewe.

Ikazidi kusemekana kwamba, wawili hao wakiwa ndani ya uhusiano, Siwema hakuwahi kumfahamisha kuwa ana mchumba ambaye ni Nay. Ikafika mahali, kigogo akamvisha pete ya uchumba, picha zikatoka kwenye gazeti moja .

Ilizidi kuelezwa kuwa Nay baada ya kugundua kuwa Siwema amevishwa pete ya uchumba na kigogo huyo, alihamanika kiasi kwamba taarifa zilimfikia kigogo huyo wa serikali naye akaamua kujitoa kwa Siwema, akaoa mwanamke mwingine.

“Tatizo Siwema hakuwa muwazi  kwa kigogo kwamba, Nay ni mchumba wake. Lakini kabla ya kigogo kumtema Siwema, kumbe alishawahi kumpiga picha za utupu mwenyewe akiwa hajui.”

“Sasa baada ya Siwema kumwagwa kutokana na kelele za Nay kwamba demu ni mchumba wake, ndipo zile picha Siwema alizitumia kumtishia amnunulie gari vinginevyo angemwanika kwa kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook,” kilieleza chanzo hicho.

Ikazidi kuelezwa kuwa, aliposikia vitisho hivyo, kigogo huyo aliamua kumweleza mkewe juu ya sakata zima ambapo walikubaliana kumnunulia Siwema gari na akampa na kiasi cha fedha kwa masharti ya kuzifuta picha hizo kutoka kwenye simu yake


“Lakini Siwema licha ya kununuliwa gari aina ya Honda CRV na akapewa na kiasi cha fedha alichotaka, bado hakuzifuta picha hizo kwenye simu yake.

“Kana kwamba haitoshi, aliendelea kumtishia tena ambapo safari hii alitaka  atumiwe kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mtaji wa biashara, jambo lilimnyong’onyeza kigogo huyo na kuamua kwenda kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria,” kilisema chanzo.

Akizungumza na gazeti la  Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Alisema Siwema alikamatwa baada ya mlalamikaji kutoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo walifungua jalada la uchunguzi Mei 2, mwaka huu na siku hiyohiyo walimkamata mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake, Lumala Manispaa ya Ilemela.

“Ni kweli tulimkamata Siwema Edson (27), mkazi wa Lumala. Ametuhumiwa kujipatia mali kwa njia ya vitisho. Awali alikuja mlalamikaji kabla ya kukamatwa.

“Hawa watu awali walikuwa wapenzi. Katika mapenzi yao, siku moja, Siwema alimpiga picha za utupu mlalamikaji bila yeye kujitambua wala ridhaa yake,” alisema DCP Mkumbo.

Alisema baadaye uhusiano wao ulivunjika, ndipo Siwema akatumia picha hizo kumtishia kuwa kama hatatimiza matakwa yake kwa kumnunulia gari na kumpa fedha, basi angezisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook.

“Mlalamikaji alitimiza matakwa ya mtuhumiwa kwa kumnunulia gari aina ya Honda CVR lenye namba za usajili T103 DDU na akamtumia na fedha. Lakini Siwema aliendelea kumtumia vitisho, akimtaka amtumie kiasi kikubwa cha fedha za mtaji, ndipo mlalamikaji akaja kutoa taarifa polisi, likafunguliwa jalada la uchunguzi na siku hiyohiyo akakamatwa,” alisema DCP Mkumbo.

Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa gari hilo linashikiliwa kituoni hapo huku Siwema akiachiwa kwa dhamana wakati upelelezi ukiendelea. Ukikamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alisaini sheria ya makosa ya mtandao.

Sheria hiyo, inakataza mtu kutumia mitandao kwa nia ya  kumchafua mtu au kuanika picha zake, hasa za utupu  bila ridhaa yake.

Chanzo: Gpl/Ijumaa wikienda

Wachaga Wamegawanyika Kama ifuatavyo, Sio Wote ni Wajanja!

Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja. Kuna:-
1. Warombo wajanja sana kibiashara/wezi pia, wameajiri Wamarangu mjini ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanawake zao ni mama Huruma, wanaachia tu.. Ukioa mrombo ujue umeolea kijiji.

2. Kuna Wamarangu wazuri sana wa sura na umbo wanawachuna Warombo. Wanawake wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu.

3. Kuna Wakibosho wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchinja... wengi wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili.. Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.

4. Kuna Wamachame hawa ni wezi sana, ukifanya nae dili umeliwa, niwasiri sana, anaweza kukuua huku akitabasamu, sio waaminifu sana lakini huenda kanisani mara nyingi zaidi kuliko Wachaga wote. Wanawake wa machame wanaitwa 'Wapalestina'.. Mume ukitajirika mkeo anakuua ili arithi mali.

5. Kuna Wauru, hawa hupenda kusoma sana lakini hawapendi maendeleo kabisa, wanawake wakifikisha umri wa miaka 40 hua wehu na wanaume huwa vichaa mapema zaidi. Wanaume ni wavivu, wanawake ni wachapakazi hodari. Wanazurura mjini na mabeseni wakiuza ndizi mbivu.. Ukioa Uru jiandae kulea kichaa.

6. Kuna Wakirua, wanapenda sifa kama Wahaya. Wanawake wa Kirua ni wachawi kupindukia.. Wanaloga hata jiwe ili tu alikomoe.. Wanaume wao hawaoi kwao.. Hawapendi kuishi mjini maana wanaogopa gharama.. lakini siku wakija mjini watatu tu utadhani wako mia.

7. Kuna Wa-old Moshi. Hawa ni mafundi stadi wa ujenzi wa nyumba, japo hawajengi kwao. Mpaka leo hamna daladala ya kwenda Old-Moshi kuanzia Moshi mjini, maana ni wabishi kulipa nauli na pesa inaishia kwenye mbege njiani. Wanaume wamezoea kutoka nyumbani saa kumi na moja alfajiri na kurudi saa sita ya usiku kwa miguu.

Meck Sadick aipongeza Mvua na Kuishukuru Kwa Kuwahamisha Wakazi wa Mabondeni!


Pamoja na mvua hizi kulaumiwa na kulaaniwa kila kona kwa kuleta madhara pamoja na kupoteza maisha ya watu, mvua hizi sio balaa kwa kila mtu bali kwa wengine ni neema na simestahili pongezi!.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick, amezipongeza mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la dar es salaam, kwa mvua hizo kuisaidia serikali katika utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu, kuwaamuru wakazi wa mabondeni kuhama kwa lazima, ambapo waligoma kata kata kuhama, na serikali ilimkuwa bado inajishauri namna ya kuwahamisha watu kwa nguvu bila kuleta madhara, haswa kwa kuzingatia huu ni mwaka wa uchaguzi!, mvua hizi zinazoendelea kunyesha zimeisaidia serikali kuwahamisha wananchi hao, hivyo Meck Sadik amezishukuru sana!.

Mkuu huyo wa Mkoa, ametoa shukrani hizo, katika mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Kumepambazika, kinachorushwa na Redio One Stereo asubuhi hii.

Amesema ametokea taarifa za kupoteza maisha kwa watu wengine wawili, mmoja amesombwa alipotaka kuvuka mto Ng'ombe maji yakamzidi nguvu na kumsomba, na mwingine ni mtoto mdogo wa miaka miwili, alikuwa akicheza nje ya nyumba yao mafuriko yakapita mbele ya nyumba na kumsomba!.

Kuhusu wakazi wa mabondeni, Mkuu wa Mkoa alisema baada ya mafuriko ya 2011, waliwahamisha na kuwapatia viwanja Mbweni, baadhi yao walihama na wengine waligoma na kwenda mahakamani ambapo serikali ilizuiliwa kuwahamisha kwa nguvu.

Hoja za wakazi hao kupingwa kuhamishwa ni kwa sababu wametumia gharama kubwa kwa ujenzi na kuwekewa huduma muhimu za maji na umeme, hivyo hawawezi kuhama bila kufidiwa!. Lakini sasa mahakama imeishatoa uamuzi lazima wahame, na serikali ilijipanga kutumia nguvu kuwahamisha, tena this time bila kuwapatia maeneo mbadala, lakini kabla ya utekelezaji wa zoezi hilo, Mungu akaleta mvua saidizi ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa kuwahamisha, hivyo kuipunguzia serikali kazi ya kuwahamisha kwa nguvu.

Mkuu wa Mkoa amesema baada ya usaidizi huu wa mvua kwenye kuwahamisha watu hao, sasa serikali imebakiwa na kazi ndogo tuu, kuhakikisha watu hao hawarudi katika maeneo hayo, na kuwasisitiza wale wote walohama na kubakiza baadhi ya vifaa vyao, mvua zikisimama wataruhusiwa kivichukua kabla ya kupitisha tingatinga na kulisawazisha eneo lote kubaki tambarare kama walivyofanya kwa eneo la Kipawa!.

Pia Meck Sadiki aliviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano katika zoezi hili kuhakikisha wakazi wa mabondeni wanahama kwa ridhaa yao kutekeleza amri ya mahakama na wale wote watakao kaidi, watahamishwa kwa nguvu.