Akizungumza na mtangazaji, Mama Nyerere alimuuliza, "ukiniangalia unanionaje?" ambapo mtangazaji alimjibu, "nakuona mzima!" huku wakitabasamu.
Mama Maria alisema huu ni mwaka wa uchauguzi, hivyo mambo haya ya uzushi si ya ajabu.
Kabla ya uvumi wa kizushi kuhusu Mama Maria, juzi kupitia WhatsApp ulikuwa ukitumwa ujumbe mwingine wa kumzushia kifo Reginald Mengi, Mwenyekiti wa makampuni ya IPP.