Mrembo na staa wa Bongo Movies ,Jaqueline Massawe Wolper
amefunguka kuwa anajua thamani yake kama msanii hivyo hawezi kutumika
na wafanyabiashara kwa kuwatangazia biashara zao bila kuwa na mikataba
ya kueleweka au mtu kumfanyia maamuzi pasipokuwa na makubaliano na
kufikia mwafaka kuhusu hilo.
“Kujenga jina katika sanaa si kazi ndogo, unapigana na
kujitoa na inapotokea maarufu watu wanaanza kuona thamani ya jina
ulilolijenga basi ni wakati wa kulilipia na si bure tena,”anasema.
Jack anasema hivi karibuni alikataa kupiga picha na kampuni
moja baada ya kutaka apige picha akiwa ameshika bidhaa mkono
wakimlaghai kuwa wamemletea zawadi pia wakitaka picha za bidhaa hiyo
atumie katika akaunti yake ya kijamii, anajua walifanya hivyo kwa sababu
ana watu wengi, lakini yeye alikataa.