Sio Kila Mhaya ana Dharau Jamani, Aliye Sema Milioni Kumi ni ya Mboga ni yeye Wengine Hatuko Hivyo

Naandika hivi nikiwa na masikitiko makubwa sana juu ya ukabila unaoota mizizi hasa katika kipindi cha hvi karibuni ndani ya nchi yetu! Hivi karibuni aliyekuwa Waziri wa nyumba na makazi mama Tibaijuika alikaririwa akisema MILIONI KUMI NI KWA AJILI YA MBOGA!

Kwa kweli hii ni dharau kubwa sana; lakini hoja yangu ni kuhusu maneno yanayoendelea kwenye mitandao mbalimbali ikiwahusisha wahaya wote na huyu MTU! Kimsingi hili jambo linanikera sana maana ni kuendekeza ukabila na ubaguzi kwani mtu mmoja hawezi kuwa KIGEZO cha kuwaamulika watu wote wa jamii husika!

Bila shaka ninyi ni mashahidi juu ya kauli nyingi zilizowahi kutolewa na watu wa aina mbalimbali hasa viongozi lakini hazikuhusishwa na ukabila! Tafadhali epukeni ukabila kwani ulileta madhara makubwa Rwanda & Burundi pamoja na Kenya! Ni hayo tu kwa Leo..