Penzi la Wema Sepetu na Ommy Dimpoz, Kumbe Dimpoz ni Boya tu Nyuma ya Pazia kuna Kigogo


HABARI ya mjini ni kwamba, lile penzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.


Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo awe mpenzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye ndiye anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.

“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma.

“Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye cha