Amanda agoma kumuweka wazi mpenzi wake kwa kuhofia mashushushu!!!


Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amefunguka kuwa anaogopa kumtambulisha bwana wake wa sasa kwa kile alichodai kuwa anaogopa kuibiwa.
 
Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’.
 
 Akizu ngumza na paparazi wetu juzikati, Amanda alisema ameishi kwa muda mrefu na mpenzi wake bila kuhitilafiana kwa sababu wengi hawamjui, lakini anahofia akimuanika wasichana wataanza kumfuatafuata na kumwiba.

“Kumtambulisha bwana wangu wa sasa sitaki, naogopa wadada wa mjini hawakawii kumzengea zengea na kuniibia hivihivi naona. Kwa mfano sasa hivi watu hawamjui basi wametuliaaa! Lakini ukimweka hadharani tu, hao,” alisema Amanda.