UPDATES: Mafuriko yanayoendelea sehemu mbalimbali za jiji la Dar es as Salaam

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejikuta tena kwenye sintofahamu kubwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha tangia jana.

Maeneo mengi hali ni mbaya kutokana na mvua kunyesha kwa wastani wa saa 14 mfululizo!

Nimetokea maeneo ya Tegeta hali ni mbaya. Nyumba zimejaa maji. Maeneo ya Mbezi kutokea Goba kuna magari yametelekezwa njiani kutokana na maji mengi. Kuna gari dogo ya Toyota (jamii ya saloon kama sikosei) Imetelekezwa hapa Mbezi tangi bovu na imefunikwa na maji yanayotokea huku ukanda wa juu! Pia nyumba nyingi maeneo haya ya Mbezi beach zimezingirwa na maji na zimetelekezwa!

Nimepita Sinza hali ni mbaya sana. Maji yapo kila kona, njia hazipitiki!

Stendi ya Makumbusho asubuhi ya leo ilikuwa na daladala chache sana.

Barabara nyingi zinaongozwa na mataa badala ya askari wa trafic. Mfano mataa ya Chang'ombe kitu ambacho ni nadra sana na ni kutokana na magari kuwa machache sana!

Nasikia pia huko Mbagala hali ni tete kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Emb tujuzane na kwa wale ambao mnaweza kuweka picha pia itasaidia