RAY C Afunguka 'Heri Virusi vya UKIMWI Kuliko Madawa ya Kulevya'


Mwimbaji Ray C Amefunguka na Kusema heri mtu anaishi na Maambikizi ya Virusi vya Ukimwi hawezi kujulikana mapema kama anavyo kwenye jamiii kuliko mtumiaji wa Madawa ya kulevya kwani haichukui muda mrefu kwa jamiii kumjua mtu anayetumia Madawa ya kulevya kwa vile tabia yake baada ya kutumia kwa muda fulani zinakufanya unapoteza mwelekeo kwa kila kitu ..

Ray C amesema Hata yeye wakati anaanza kutumia Madawa ya kulevya palikuwa na tetesi lakini alizikana kwa nguvu sana kila mahali ikiwemo na kwenye vyombo vya habari..lakini ilifika muda akaanza kupoteza mwelekea kutokana na kuzidiwa kwa madawa ya kulevya ...

Ray C anasema Mwisho wa kutumia Madawa ya kulevya huwa ni AIBU hivyo Vijana Waepuke Aibu hiyo......