Pedeshee Jack Pemba Azua Tafrani Dar..Afanya Vurugu Airport, Ajigamba Amerudi Bongo Adai Kina Wema na Aunty Ezekiel Hawana Jipya


Kijana Jack Pemba amezua kizaazaa uwanja wa ndege Dar. Hii ni baada yakuanza kuvamia meza za watu na kujitangaza kuwa amerudi Dar.

Huku akiongea kwa sauti kubwa hadi bar yote ya Flamingo ikisikia, Jack alitoa lugha za matusi kwa wageni wote walikuwa katika bar hiyo. Jack alijigamba pia kuwa kina Wema na Aunt Ezekiel hawana jipya kwake na ndio amesharudi Dar kusumbua mji.

Maaskari wamekuja na kutaka kumsweka ndani ila Jack akaomba msamaha na watu wengine wamemuombea msamaha.
Ndipo jack kaamua Flamingo nzima wapewe vinywaji na yeye analipa. Kabla ya bili kuja jack kamwaga madolari mezani.

Inaonekana Jack ana stress za maisha.