Nay wa Mitego "Shamsa Ford Akitulia Namuhalalisha Kuwa Mke Wangu Kabisa"


Staa wa Bongo Fleva,  Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, ameeleza kuwa endapo staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford  ambaye sasa hivi wanapika na kupakua,  atamuonesha utulivu na uaminifu hataona sababu ya kutomuoa.

Nay aliyasema hayo juzikati alipokuwa akizungumzia mipango yake na Shamsa ambaye amejiweka kwake baada ya kutosana na mzazi mwenzake, Siwema. Nay alisema:

 “Hilo la ndoa kiukweli kabisa kama Shamsa ataonesha kutulia na kunithibitishia kuwa hatakuja kunizungua, sitaona hatari kumuoa.”

GPL