Mgomo wa wafanyakazi wa mabasi yanayotoa huduma jijini Dar es Salaam,
leo asubuhi umesababisha mtafaruku mkubwa kwa wakazi wa jiji hili ambapo
wengi wao walionekana wakitembea kwa miguu kuelekea kazini na katika
shughuli zao mbalimbali.
Mgomo huo ambao unaenda sambamba na usafiri wa mabasi ya abiria nchi
nzima, unafuatia ule uliotokea Aprili 11 mwaka huu, ambapo wenye mabasi
na wafanyakazi wanataka maridhiano na serikali katika masuala
mbalimbali.