Staa wa Bongo Movies mwenye mvuto wa aina yake, Ester Kiama ameibuka na
kuwachana mastaa wa kike wanaopenda kuiba waume za watu kwamba waache
kwani si tabia nzuri.
Akizungumza na GPL Ester alifunguka kuwa mastaa wanaochukua waume za
watu, tabia zao siyo nzuri na kibaya zaidi wakishawachukua wanajigamba
ili watu wawaone wako juu mjini wakati hawana lolote.
“
Siyo kwamba sijawahi kuwa na mume wa mtu, nilishawahi lakini
nimetokea kuwachukia sana kwani hawana faida zaidi ya kuwapotezea
wasichana muda wao, nimejifunza mengi na sitarudia tena hivyo nawasihi
wenzangu waache kuiba waume za watu kwani watarogwa tu,” alisema Ester