Wema: Mama Yangu Amepoteza Uwezo wa Kuona Kwa 75%!


Staa wa Bongo movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa mama yake mzazi, Miriam Sepetu anasumbuliwa na macho ambapo madaktari wamegundua kwamba amepoteza uwezo wa kuona kwa asilimia sabini na tano (75%).

Kwa mujibu wa Wema, aliamua kumpeleka mzazi wake huyo hospitalini (hakuitaja) ndipo alipohakikishiwa tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

“Kumnusuru mama yangu asipate upofu wa moja kwa moja inabidi afanyiwe operesheni ya macho,” alisema Wema kwa huzuni kwa kuwa hakuna kama mama.

Kwenye ukursa wake mtandaoni  Wema aliandika "My mumumu anaumwa macho and she is abt to have an eye surgery... You'll be fine inshallah my love... I love u with all my heart..."mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu akiwa na mama yake.

Pole sana mama Wema.