Mh. Zitto Tunakuomba Ugombee Ubunge Jimbo la Ubungo

Mimi nikiwa Mwananchi na mkazi wa Ubungo makoka nakuomba mh zito uje ugombee jimbo la Ubungo kutokans na kero hizi:

1. Mbunge wangu ameshindwa kwa kipindi cha miaka mitano ameshindwa kutatua matatizo ya maji. tunakaa mwezi mzima hatuna maji ni mateso
2. Barabara zetu mbovu hasa hii ya makoka Ubungo imefikia asubuhi nawakataa RAIA kenye gari yangu kwani barabara ni makorongo tupu na mbunge hatumuoni
3. Shule yetu ya kata hapa inashida nyingi mbunge kapotea wala kutembelea kutoa ushirikiano
4. Kuna shida ya daraja eneo la unyamwezini baadhi ya watu wamekufa mvua zinaponyesha kwa kupita juu ya Bomba la dawasko na mbunge hatujapta muona hata siku moja ni majanga
5. Vijana wengi wa Ubungo ajira hawana wanapanga vitu jioni kwenye transfoma za umeme Ubungo mbumge ameshindwa kutoa njia mbadala ili vijana wasikae maeneo hatarishi

6. Wananchi wa manzese wamesahau km wanambunge hajswahi tembelea ht ck moja. mitaro imeziba nyumba zimejaa maji kipindi hiki cha mvua mbunge wetu hana ht habari

Niishie HP kiukweli ninamengi sana mbunge wangu amefeli mtihani sizani tutampa tena nafasi.
Mh Zito njoo utuokoe sisi wakazi wa ubungo

By assadsyria3/JF