Mgomo...! Mgomo..! Mabasi Yote Ya Abiria Yapanga Kugoma Nchi Nzima


WAMILIKI wa Mabasi yaendayo mikoani wameitunishia misuli Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA )na kusema kuwa hawatashusha nauli kutokana na bei ya mafuta kupanda.

Wamesema kama SUMATRA hawatatoa  majibu mapema kuanzia  Aprili 29 mwaka huu hawatokata tiketi kwa wasafiri na badala yake wataendelea na mgomo huo kwa  siku saba.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana  katika kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani , Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema SUMATRA ilikurupuka  kushusha nauli bila kufanya mchanganuo na kuda.

Wamiliki hao waliafikiana kuwa yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara kabla hawajapata muafaka kutoka SUMATRA watamchukulia hatua za kisheria.

TABOA wameitaka serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani kwenye hali yake ya kawaida iliyokuwepo miezi michache iliyopita kwasababu bei ya mafuta imerudi juu, baada ya kushuka kwa kisingizio cha bei ya mafuta kushuka