Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Dar es Salaam jana, Jini Kabula alisema kuwa ni filamu chache zinazofanya vizuri sokoni, ikiwemo ya Chozi la Wanjaa iliyochezwa na Aunt Ezekiel, Kulwa Kikumbi ‘Dude’ na wasanii wengine ambazo zinaonekana kuwafurahisha watu, isipokuwa nyingi zinatengenezwa kwa kulipuliwa.
“Hakuna haja ya kumtafuta mchawi wa anguko la filamu nchini, kwani wengi wanatengeneza kwa kulipua, endapo waandaaji wasipobadilika, fani hii itakuwa haina maana tena kwa waigizaji,” alisema