|
Shilole na Nuhu Mziwanda |
Story ya kwenye U Heard ya leo March 10, inahusu tetesi zilizoenea kuwa
wa dada wa mjini akiwemo muigizaji, Jacqueline Wolper wamemchoka msanii
Shilole kwa madai kuwa amekuwa akimpiga mpenzi wake Nuh Mziwanda mara
kwa mara na wanataka kumtafutia mpenzi mwingine ambae hatampiga, mpango
uliopangwa siku ambayo Shilole alimpiga Nuh na wasanii waliokuwepo
kuingilia.
Soudy Brown amemtafuta Shilole na kumpa taarifa hizo na kusema sio kweli
ila watu wanazusha ili kuwagombanisha jambo ambalo hawatafanikiwa kwa
kuwa anajiamini sana, kwa upande wa Nuh amesema kuwa ndio kwanza
anasikia taarifa hizi ila mwanaume huwa hatafutiwi mwanamke na Shilole
hampigi kama wanavyodai zaidi ya kuishi kwa raha.