Tanzania Yapaa Wiwango vya Mpira FIFA

Tanzania imepaa kwenye viwango vya kila mwezi vya FIFA kwa kupanda kwa nafasi saba (7)  katika viwango vya shirikisho hilo la kimataifa vilivyotolewa leo.
Rwanda ndiyo imetia fora kwa kupanda kwa nafasi nane (8) na kuongoza Afrika Mashariki ikiwa nafasi ya 64 duniani ikifuatwa na Uganda (74), Tanzania, Kenya (118) na Burundi (126).

Algeria wanaendelea kushikilia usukani Afrika wakifuatwa na Ivory Coast, Ghana, Tunisia, Senegal, Cape Verde, Nigeria, Guinea, Congo DR na Cameroon wanaokamilisha 10 bora barani.

10 bora duniani inaendelea kuongozwa na Ujerumani wanaofuatwa na Argentina, Colombia, Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ureno, Ufaransa, Uruguay na Italia waliopanda kwa nafasi mbili na kuitoa Hispania.