Siri ya Diamond Kuhamia Kwenye Nyumba Yake Mpya Fasta Fasta Yangundulika

HATIMAYE siri ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuhamia kwenye mjengo wake wa kisasa uliyopo Tegeta -Madale jijini Dar imevuja huku ikitajwa kuwepo na vionjo vya ushirikina.

Chanzo makini kimeliambia Amani kuwa, licha ya kumalizika kwa mjengo huo, lakini Diamond alikuwa akikataa kuhamia kutokana na umbali kutoka huko hadi mitaa aliyoizoea lakini shinikizo lilikuja kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Zarina Hassan ‘Zari’  ambaye tangu aliponasa ujauzito amekuwa akitamani kuwa karibu na mpenzi wake huyo ila ilikuwa ikishindikana kufuatia mazingira aliyokuwa akiishi mwanzo Diamond, Sinza-Mori, D

“Ndugu yangu kama unataka kufahamu undani zaidi wa hiki ninachokueleza muulize Diamond mwenyewe atakwambia, Zari siku zote alikuwa akitaka kuwa karibu na Diamond, hasa baada ya ujauzito lakini ndugu zake walikuwa wakimkatalia kufanya hivyo kwa kuhofia mimba yake kuchoropoka kutokana na vijicho vya watu.

Jumamosi iliyopita, Diamond alikata shauri na kuhamia kwenye makazi yake mwenyewe baada ya ujenzi wa miaka karibia mitatu. Kwa mujibu wa mkandarasi mmoja, nyumba hiyo mpaka kukamilika kwake, imetafuna karibu shilingi milioni mia nne (400,000,000).
GPL