Shamsa: Sipendi Wanaolalamika Kutendwa!

Mrembo na mwigizaji wa filamu mwenye mvuto wa aina yake, Shamsa Ford leo mtandaoni ametoa mtazamo wake kuhusu swala la watu kulalamika muda wote kuwa  wametendwa kwenye maswala la mahusiano ya kimapenzi.

“Huwa sipendi watu wanaolalamika kutwa kwamba wametendwa bila kuangalia nyuma yeye kawaumiza wangapi ambao waliamua tu kumnyamazia na kumpuuza”.

Wengi walionyesha kumuunga mkono kwa kubonyeza kitufe cha kupenda na wengine kushusha komenti zao, Je wewe kwa upande wako swala hili unaichukuliaje?.