Maneno Haya ya Faiza ni Darasa Tosha wa Wanawake Wengine

Staa wa Bongo Movies Faiza Ally ambae ni mzazi mwenza wa Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amebandika hili andiko hili mtandaoni, hebu chukua muda wako kulisoma andiko hili, kuna punje utazipata.

Nimepata marafiki wengi wapya - na wengine ni baada ya kuona kipindi kinacho endelea Jana (juzi) na leo (jana) Claud's TV - nataka tu niwaambie kwamba wakati huo wa uzuni na uchungu mwingi ulisha pita sasa hivi niko sawa kabisa na nimekubali matokeo ya maisha yaliopo sasa- na zile tofauti haziko tena na baba mtoto japo hatuko pamoja .    

Niwaambie tu kitu kimoja ni kwamba wakati unapo kuwa ktk wakati mgumu wa maisha unakua unaona kama haupiti na kipindi cha siku unaweza ukaona ni Kama mwaka kwa ule uchungu ulio nao- na pia unaweza unafanya Mengi kupitia wakati huo .

Faiza Ally
 Lakini cha msingi na muhimu usijasahau wewe ni nani na una thamani gani ktk maisha yako, ni kwamba lia futa machozi na uendelee na maisha yako - hakuna atakae badili maisha yako zaidi ya wewe - usikubali uchungu uka haribu maisha yako yote.

Jikaze simama na usonge - muweke Mungu karibu fanya vitu unavyo penda basi taratibu utarudi ktk hali yako ya kawaida na usimn'gan'ganie mtu asie kutaka atakuumiza zaidi hata kuhurumia kabisa  mwanaume ni mzuri pale anapo kuhitaji wewe Lakini akikuchoka hawezi kukumbuka hata jambo lako 1 zuri yote yatakua mabaya .. Lakini usiumie sana japo yanaumiza usijione hufai kwa ajili ya mtu mmoja mwingine akikuona wa nini wengine wanasema tutampata lini.

 Sasa nina furaha uchungu wa mapenzi uliisha na hauna nafasi tena kwenye maisha yangu nawaza mambo muhimu tu juu ya mwanangu maisha yangu na watu wangu wanao nikubali .... Basi msinipe pole tena maana nimechoshwa na pole kwa kweli - Asenteni- Faiza alimaliza.

 Asante Faiza kwa kushare nasi experience yako kuna watu wamejifunza kitu hapa, kila la kheri kwenye maisha yako.

Mzee wa Ubuyu