Breaking News: Ajali Mbaya Iringa Kontena Laangukia Basi la Abiria

Hizi safar hizi...jaman ukipanda gar unashukuru na ukishuka salama pia husisahau kushukuru....  Amjali imetokea changalawe mafinga basi la Majinja limeangukiwa na kontena muda huu hali si nzuri.... Inasemekana watu Karibia wote Wamapoteza maisha.....MUNGU AZILAZE MAHAL PEMA PEPON ROHO ZA MAREHEM JAMAN.....DUH...
Updates 

Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lililolaliwa na lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.