Anna Makinda 'Siwezi Mfukuza Zitto Kabwe Bungeni'

Ana Makinda
Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hawezi kumtangaza Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kuwa siyo mbunge hadi atakapopata barua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ameongeza kuwa hawezi kufanyia kazi taarifa za kwenye vyombo vya habari, badala yake anasubiri taarifa za kiofisi kutoka NEC. Kwa upande wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa, amesema bado hawajaandika barua kuiarifu Nec, kwa kuwa hilo siyo jambo kubwa ambalo chama kinapaswa kuhangaika nalo kwa sasa
Nini maoni yako katika hilo?