Watuhumiwa wanne wa Amboni wakamatwa na wananchi wakishirikiana na JWTZ

Wananchi wa Mleni, Amboni mkoani Tanga, kwa msaada wa askari wa JWTZ, wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wanne wanaotuhumiwa kwa ujambazi na ambao walikuwa wamejificha katika mapango ya Mleni huko Amboni Tanga.

Kwa mujibu wa ITV,wananchi waliwaona watuhumiwa hao na kisha wakawaapigia simu askari hao wa JWTZ ambao walikuja kuwakamata na kisha kuwakabidhi Polisi.

Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Jeshi hilo,afande Chagonja ameahidi kuwa, raia waliosaidia kukamatwa kwa wahalifu hao watapewa zawadi,zawadi ambayo ameifananisha na "takrima".

Watuhumiwa hao wameelezewa kuwa ni wenye asili ya "kiarabu" na "kisomali" na kwamba walikamatwa wakiwa wamedhoofika kwa njaa.

CHANZO: ITV