Uteuzi wa Makonda ni fimbo kwa mafisadi.Asibezwe anaweza.
Anaitwa Paul Makonda.Ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Uvccm.Kijana
mdogo mwenye ujasiri wa kipekee asiyeogopa kejeli,dharau na fitna za
mafisadi.Kwasasa ndio Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.
Jamii ya wenye akili inashangaa wanaobeza uteuzi wa rais kwa Paul
Makonda.Inawashangaa wanaomponda Paul Makonda.Haijajulikana hadi sasa
nia na sababu zenye mashiko zinazotumika kumchafua Paul Makonda.Vijana
wanaombeza ndio haohao wanaoomba kila siku kuwa vijana wapewe nafasi
katika vyombo vya maamuzi.
Kumponda Paul Makonda ni kudharau uteuzi wa rais wa nchi.Rais anatambua
umuhimu wa vijana kupewa nafasi.Anatoa fursa kwa vijana.Hili ni jambo la
kupongezwa sana.Ni hatua kubwa na nzuri kwa ukuwaji wa demokrasia
nchini.
Paul Makonda kaaminiwa.Mnalalamika kila siku kuwa kina January na
Kigwangallah au Mwigulu wasibezwe tena wao wanaomba nafasi kubwa ya
urais.Lakini Paul Makonda kupewa Udc mnaona kama kapendelewa na
hawezi.Sisi tunaamini Paul Makonda anaweza na wilaya aliyopewa aiongoze
ataimudu,aungwe mkono kwa asilimia mia moja.
Kelele za mafisadi zisiondoe imani kwa vijana wasiowaunga mkono.Paul
Makonda anapinga ufisadi.Ni jasiri.Mpiganaji wa kweli dhidi ya
maovu.Kambi za urais zisiwapotoshe.Wanaomsema hovyo wamepoteza dira ya
kisiasa na kimaisha.Wana political stress isiyotibika inayotokana na
kukosa maadili ya uongozi na kisiasa.
Abarikiwe Paul Makonda.Abarikiwe aliyemteua.Ibarikiwe Ccm.Ibarikiwe Tanzania.Ibarikiwe Kinondoni.Viva Paul Makonda "Jembe".