Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alitaja tukio hilo ni la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa kata ya Nyakata Bukoba vijijini.
Alimtaja aliyeuawa ni Pelagia Martin (46) aliyeunguzwa mwili mzima. Kamanda alisema mwanamke huyo alicheleweshwa kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize bila kwenda Polisi.
Makubaliano ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba Amelia alimfumania Pelagia akiwa na mumewe, Richard Bulebo (57) ndani ya nyumba yao.
Kwa mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa mbaya, ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba msaada.
Polisi walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki kabla ya kupatiwa matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.