Mwanamitindo Flaviana Matata Kuolewa Mwaka Huu

GOOD news kutoka kwa Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata ni kwamba anatarajia kufunga pingu za maisha Agosti 15, mwaka huu na kijana wa Kichaga anayejulikana kwa jina la Deo Masawe aishie Atlanta, Marekani.

Chanzo makini kutoka Atlanta, kimesema taratibu zote zimeshafanyika na kilichobaki ni siku ifike watu washerekehe.

“Nadhani kwa mwaka huu ndiyo itakuwa harusi ya kwanza ambayo itaacha historia kwa kuwa waoaji wamejipanga kisawasawa,” kilisema chanzo chetu huku mtu wa karibu na Flaviana akithibitisha tukio hilo na kudai litakuwa la kihistoria.