MANAIKI: Bado Sijakata Tamaa Kumuoa Jack Wolper

Mwigizaji wa filamu mwenye mikasa ya aina yake, Manaiki Sanga  ‘The Don’ amesema kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii mwenzake, Jacqueline Wolper na kwamba bado anaendelea kuwashawishi wazazi wake.

Akiongea na Gazeti la Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado anawashawishi wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu anayempenda.

“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema Manaiki.

Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.