Dully Sykes Alaumu Wasanii Ambao Hawakuja Kumzika Baba yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, ameshangazwa na kitendo cha wasanii wengi kutojitokeza katika mazishi ya baba yake mzazi, Ebby Sykes

“Nilitegemea kwakuwa tunampumzisha baba yangu hapa hapa Dar es Salaam, wangekuja wasanii wengi ambao ni marafiki zangu, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa,” .

“Sijui walijua nitakuja kuwaomba fedha zao, mimi nilishapata michango mingi kutoka kwa watu wengine mbalimbali, ukweli wasanii tuache roho za kimasikini,” alisema.

Sykes aliendelea kusema amegundua asilimia kubwa ya wasanii wamekuwa wakipendana wakati wa raha tu, lakini inapofika muda wa matatizo kila mmoja hukimbia.