HII
ni ‘bad news’ kwa staa namba moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’. Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda anayefahamika kwa jina
la King Lawrence, ameibuka na kumuita nyota huyo shoga, Ijumaa linakupa
habari hii.
Staa namba moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan ‘Zari’.
ISHU ILIPOIBUKIA
King ambaye ana makazi yake pia nchini Afrika Kusini, amedaiwa kutoa
kauli hiyo juzi, Jumatano kupitia mtandao wa Facebook akionesha kukerwa
na kitendo cha staa wa muziki Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ kuangukia
katika penzi la Diamond.
ATUMIA GIA YA WATOTO
Awali, King ambaye imeelezwa alikuwa na urafiki na dereva wa
aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga, alianza kwa kumchokonoa Diamond
kwa gia ya kujifanya anawatetea watoto wa Zari ambapo alitupia picha ya
Zari akiwa na Diamond mtandaoni ikiwa na ujumbe wenye kejeli na jeuri ya
fedha.
UJUMBE ULIVYOSOMEKA
“As a concerned uncle, Im offering Zari’s tomboy Diamond Dola 40,000
so as to leave the old mom of three to take care of her kids. The young
boys miss their mom. Please Diamond do it for the kids.”
(Nikiwa kama mjomba, ninampa jikedume wa Zari, Diamond, Dola 40, 000
(Sh. Mil 66) ili amuache mama wa watoto watatu (Zari) awalee vizuri
watoto wake. Watoto wanammisi mama yao.”
Diamond Platnumz na Zari wakidendeka.
ABADILISHA GIA
Kuonesha ana mpango mchafu wa kumchafua Diamond ambaye anaipeperusha
vyema bendera ya Afrika kimuziki, badala ya ishu ya watoto, alibadili
upepo na kujinadi eti yeye ndiye wa kwanza kutembea na Zari.
Pasipo kueleweka kusudi lake, alimpiga dongo Diamond ambaye usiku wa
kuamkia leo alipewa heshima ya kipekee kutumbuiza kwenye Tuzo za
Wanamichezo Bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Afrika (Caf) nchini
Nigeria.
HEBU MSIKIE
“Kwa nini utembee na Diamond shoga? Sijui kama anajua kwamba mimi
ndiyo wa kwanza kutembea na wewe (Zari),” aliandika katika mtandao wa
Facebook. AZIDI KUTAPATAPA
Kama hiyo haitoshi, kupitia mtandao wa Facebook, King alitupia
mawasiliano yake ya zamani na Zari akidai alikuwa akimuomba fedha.
DIAMOND ANASEMAJE?
Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kumpata Diamond ili aweze
kujibu tuhuma hizo hazikuzaa matunda huenda ni kutokana na ubize
aliokuwa nao katika maandalizi ya shoo hiyo kubwa Afrika, simu yake
iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.
King Lawrence.
ZARI AMSAFISHA DIAMOND
Kupitia mtandao huo, Zari naye aliibuka na kumtetea Diamond
akimwambia King ana chuki binafsi kwani hapendi kumuona akiwa na
furaha.
“Hatuna muda wa kukujadili, unafikiri Diamond anaweza kuwa shoga?
Unafikiri anaweza kubishana na wewe? Kweli nimeamini, watu wakikuona una
furaha, wanaanza kukuchukia,” alijibu Zari maneno hayo ambayo pia
ameyaweka katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram.
DIAMOND NI SHOGA?
Kutokana na madai hayo ya King, baadhi ya wadau wakubwa wa muziki
Bongo walikanusha vikali madai hayo kwa kudai jamaa huyo ana lengo la
kumchafua Diamond kwa kuwa kwa sasa anafanya vizuri Afrika nzima.
“Hana lolote huyo King, anatafuta kiki za kipuuzi, atamuitaje Diamond
shoga? Amewahi kumuona akifanya vitendo hivyo? Wivu tu wa maendeleo,
aache Diamond na Zari wafanye yao, apeperushe muziki wetu nje ya
Afrika,” alisema mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe
gazetini.
KING ANATESWA NA WIVU?
Licha ya awali King kutoonesha kwamba aliwahi kutembea na Zari,
katika maelezo yake ya pili yameonesha dhahiri kwamba anasumbuliwa na
wivu wa mapenzi kutokana na kujinadi kuwa yeye alikuwa wa kwanza
kutembea na Zari.
“We huoni ameanza kwa kujifanya anawatetea watoto, mara akajifanya
rafiki wa dereva wa Ivan mara tena amegeuka anadai alikuwa wa kwanza
kutembea na Zari hana lolote wivu tu unamsumbua atakuwa alimtaka mtoto
mzuri akamchomolea,” aliandika mdau mmoja katika mtandao wa Instagram.
KING NI NANI?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, jamaa huyo ni mfanyabiashara maarufu
nchini Uganda na Afrika Kusini na amekuwa akijinasibu kuwa na uhusiano
na mastaa mbalimbali wa Uganda akiwemo mwanamuziki Julia Kanyomozi.