Wastara Amfichua Pepo Mchafu Wa Bongo Movie!!!



Msanii anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu Bongo, Wastara Juma.MSANII anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kwamba tasnia ya filamu kwa sasa inaonekana kama imeingiliwa na pepo mbaya kutokana na mambo kwenda ndivyo sivyo kila kukicha.

Akizungumza na gazeti hili, Wastara alisema tasnia ya filamu imekuwa ni ya migogoro, chuki huku bei ikishuka jambo ambalo siyo sahihi kwani litawarudisha nyuma wasanii wakati hata kazi hiyo hailipi kihivyo.

“Mimi sitengenezi filamu mpaka nielewane na bosi bei kabisa lakini vinginevyo ndiyo maana nimeamua kujikita kwenye biashara ili niweze kuendeleza maisha ya kila siku maana tasnia haieleweki sasa hivi, naona kama pepo mbaya ametuvamia inatakiwa tumuombe Mungu sana,” alisema Wastara.