.
Katibu
wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari mapema
leo akifafanua kuhusiana na ripoti na maadhimio ya kikao cha kamati kuu
cha CCM kilichofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui
mjini Unguja kisiwani Zanzibar.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jana tarehe
13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi
wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao
chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-
1. SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW.
Chama Cha
Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa
muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na
yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali
na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya
swala hilo.
ii). Kamati Kuu
imewataka wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa
dhamana zao, na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za
kuwawajibisha.
iii). Aidha
Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili
kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la
Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati
Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji
wa agizo hilo.
2. WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
Itakumbukwa kuna
makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa
maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais,
watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.
Baada ya muda wa
adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia
mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia
mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.
3. SOKO LA MAHINDI.
Kamati Kuu
imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya
tathimini na uchambuzi, pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati
Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya
Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi
wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha
zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.
4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
Kamati Kuu
imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.Aidha
ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa
na vikao vijavyo vya Chama.
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicit