Kauli nisiyopenda Kuisikia "Wenye akili wako Chuo cha UDSM, Huko Kwingine Utachelewa Sana Kuajiriwa Ukimaliza Chuo"


Nikiwa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu Cha Tumaini- Iringa(sasa wanakiita University Of Iringa); nilikutana na "brother" mmoja aliyekuwa ndio kwanza ametua nchini baada ya kumaliza digrii yake katika chuo kikuu cha Makerere cha nchini Uganda. Akaniambia kauli ya ajabu sana, akasema, "Kwa nini umeenda kusoma chuo hicho?(akimaanisha Tumaini). Wenye akili wako UDSM, huko Tumaini umeingia choo cha kike, utachelewa sana kuajiriwa". Nikamwangalia weeee, (nikamuhurumia na kumdharau ndani kwa ndani) halafu nikamjibu; "Brother, wenye akili ni wale wenye hela za maana; wanaweza kuwa wamesoma huko UDSM ama chuo chochote na wanaweza kuwa hawakusoma kabisa!. Kujidhania una akili za kufaulia mitihani halafu usiwe na hela za maana(au atleast za kutosha) huo ni ujuha." Akiwa bado anashangaa-shangaa nilichomwambia, nikamuongezea;

"Kwanza wanaohangaika na CV za mavyuo ni wale wanaotaka kuwavutia wenye akili(waajiri) ili wawaelekeze cha kufanya(yaani wawaajiri). Mtu mwenye maono ya kujiajiri hahangaiki na CV za mavyuo bali anaangalia maarifa ya kumsaidia na kimsingi anaweza hata asiende shule bali akayapata maarifa hata mtaani tu". Akaniuliza, "Unamaanisha nini?" Nikamwambia, "Umesoma chuo Kikubwa lakini bado una akili za kikoloni zinazowaza kuwa hakuna maisha ya maana mpaka uajiriwe. Kusoma ni jambo zuri na kuajiriwa sio jambo baya lakini usikariri kuwa hakuna maisha pasipo kuajiriwa; na usifikiri kila anaefika chuo kikuu anawaza kuajiriwa tu. Siku hizi mafanikio kimaisha hayamo katika CV ya chuo ulichosoma na kamwe hutatajirika (au atleast kuwa na pesa za maana) kwa kutegemea mshahara pekee". Ikiwa imepita miaka sita sasa, sijajua hali ya kiuchumi na kimaisha ya yule brother; lakini ikiwa hajabadilisha ile "mentality" nina uhakika atakuwa "ni mbangaizaji tu" kiuchumi na kimaisha kwa ujumla licha ya kuwa anamiliki cheti cha digrii kutoka Makerere!

By Albert Nyaluke Sanga