MSANII wa filamu anayetamba na Filamu ya Chausiku, Shamsa Ford
amewafungukia watu wanaoeneza taarifa kuwa ameachana na mumewe, Dickson
Matoke kwamba hakuna kitu kama hicho.
Akizungumza na Uwazi, Shamsa alisema kuwa hajaachana na mumewe huyo na
wote wanaosema hivyo watakuwa wanamtaka.“Bado nipo na mume wangu tena
kajaa tele, nashangaa hao wanaosema kuwa tumeachana labda wanamtaka,”
alisema Shamsa.