Rais Kikwete amesema serikali haiwezi kuanzisha wala kuiendesha na
kuihudumia Mahakama ya Kadhi na ameongeza kuwa hilo ni jukumu la
Waislamu wenyewe na kwamba hawazuiliwi kuianzisha Mahakama hiyo na
kwamba hayo ndio yalikuwa makubaliano.
Pia,Rais Kikwete amesema tamko la viongozi wa dini kuhusu suala la
katiba mpya, limemshangaza, limemfedhehesha na kumsikitisha sana.
Rais Kikwete ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya amani cha viongozi wa dini wa mkoa wa Dar-es-salaam.
Chanzo: ITV