Mwanasheria Albert Msando Afunguka kuhusu Kufukuzwa Zitto Kabwe Chadema


Mwanasheria ambaye pia ni diwani kupitia CHADEMA, Ndugu Albert Msando amehoji yafuatayo;

1. Amehoji je, kama CHADEMA kinasema ni Cha Kidemokrasia kwanini kinaaamuru Afukuzwe tu kwa kuwa ameenda mahakamani?

2. Amehoji je, ni nani mwenye mandate ya kumvua mwanachama uanachama wake.

3. Je, uamuzi wa kumvua uanachama ulipaswa kutangulia kwa umma au kwa Zitto kwanza?

4. Amehoji je, imekuwaje mtu anayesimamia sakata la Escrow afukuzwe kwa sasa?

5. Amesema pia kuwa Zitto hana haja ya kubaki CHADEMA kwa kuwa hata akiomba kubaki haitakuwa na mashiko. Pia ameuliza itakuwaje akae meza moja na Tundu Lissu,Wakati Tundu Lissu anatangaza amesema walishamfukuza toka mwaka jana. Naye anaona kuwa Zitto hahitajiki CHADEMA.

6. Pia amesema lengo la kumfukuza Zitto limefanywa kinafiki tu.

7. Amesema kuwa haoni haja ya kulazimisha kila mtu awaze kama Tundu Lissu au Mbowe au Slaa.

9. Pia amesema kuwa mgogoro huu ni funzo kwa Zitto, Wanachadema na Watanzania kujua aina ya viongozi walionao.Pia amesema kuwa migogoro hii isitumike kujenga chuki.

Chanzo: Clouds TV