Hali ya Mama Yake Diamond si shwari, Diamond Agoma Kusema lolote

TUMUOMBEE! Afya ya mama mzazi wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz, Sanura Kassim ‘Sandra’ bado si shwari juzikati hali yake ilibadilika ghafla na kuilazimu familia yake kumkimbiza katika Hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini Dar ambako amepewa kitanda, Ijumaa limetonywa.

Diamond alipotafutwa kuzungumzia afya ya mama yake aligoma kusema lolote zaidi ya kuomba aachwe kwani wanao uwezo wa kuzungumzia mambo mengine bila kugusia kuhusu mzazi wake.“Naomba unipe muda maana nina matatizo sana, hata kuzungumzia ishu hiyo nadhani hakuna haja,” alisema Diamond.