Bondia Mohamed Matumla Ashinda Pambano la Ngumi Dhidi ya Mchina Wang Xin Hua Jana

Bondia Mohamed Matumla amemchapa mpinzani wake raia wa China, Wang Xin Hua kwa pointi. Matumla ameshinda pambano hilo la kuwania ubingwa wa dunia wa WBF la raundi 12 uzani wa Bantam lililopigwa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam usiku huu.