Wema Sepetu Auza Gari Alilopewa Zawadi na Diamond, Adai Hataki Kuanza Mwaka na Gundu



Wema Sepetu na Diamond Enzi za Mapenzi Yao
Lile gari jipya aina ya Nissan  Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Gorgeous Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limezua mapya ambapo baada ya kudai linamchefua sasa anadaiwa kuwa analiuza kwa kigezo kwamba hataki gundu mwaka huu mpya wa 2015.
Inasemekana kwa sasa gari lipo kwa dalali analitafutia mteja wa fasta fasta as Wema Hataki Kulisikia kabisa wala kulitia machoni.