Tanzania ya leo inamuhitaji Nyerere kuliko ilivyowahi siku za nyuma

Leo hii hakuna anaeweza kuthubutu kumkemea raisi wa Tanzania pale anapokosea.
Leo hii hakuna kiongozi wa CCM anaeweza kusimama juu ya chama chake na kutetea maslahi ya umma na si chama chake.
Leo hii hakuna kiongozi anaeweza kukemea ufisadi na wananchi wakaamini maneno yake.
Leo hii hakuna kiongozi anaeweza kutoa kauli na umma ukaiheshimu.


Leo hii hakuna kiongozi anaeweza kutoa hotuba na wananchi wakawa na hamu ya kumsikiliza.
Leo hii hakuna kiongozi anaeweza kuhutubia na watu wa mataifa mengine wakaacha shughuli zao na kumsikiliza.
Leo hii hakuna kiongozi anaeweza kukemea rushwa na ufisadi hadharani bila yeye mwenyewe nafsi yake kumsuta na kuona aibu.
Leo hii hakuna kiongozi anaeweza kustaafu na bado hotuba zake zikaishi katika mioyo ya watanzania.
Leo hii kila kiongozi akiingia madarakani, kesho yake wananchi wanaomba muda wake uishe aondoke madarakani.
Leo hii kila kiongozi akistaafu basi nae anasahaulika jumla ndani na nje ya nchi.
Inasikitisha sana!