Profesa Lipumba Akimbizwa Hospitali, Presha Yamshuka Ghafla Akiwa Mahakani

Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba amekimbizwa leo Hospitali ya  UN Clinic ya Kinondoni, Dar,  baada ya presha kushuka akiwa makao makuu ya polisi kujibu shutuma za kuandamana jana.
Lipumba  alikamatwa  jana  na  jeshi  la  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  wakati alipokuwa akielekea eneo la Zakhem, Mbagala, kulikokuwa kumeandaliwa mkutano wa hadhara, kutoa taarifa kwa wafuasi waliokuwa wamekusanyika, kuwa mkutano na maandamano yamezuiliwa na Polisi