Sheddy Clever: Nimelipwa pesa nyingi sana kutayarisha wimbo wa Diamond na Ne-Yo


Producer Sheddy Clever wa Burn Records amesema kuwa amepata pesa nyingi alizolipwa na Diamond kutengeneza collabo yake na Ne-Yo, kiasi ambacho ingemchukua miezi mitatu kuipata kwa kazi zake za kawaida za production.

Sheddy ambaye ndiye producer anayepika collabo ya Diamond na Ne-Yo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa Afrika, ameiambia Bongo5 kuwa hajawahi kulipwa kiasi hicho cha pesa toka ameanza kufanya production.

“Hii kazi tuliyoenda kufanya juzi nimelipwa, na nimelipwa vizuri tu…sijawahi kulipwa hivyo kwakweli yaani nafurahi sana,” alisema kwa furaha.

“Diamond ni msanii tofauti sana na haogopi kuwekeza katika kazi zake kwasababu anajua nini anachokifanya…Nimelipwa vizuri japokuwa kazi bado sijamaliza lakini nimelipwa pesa nyingi tu nzuri nimefikia hoteli nzuri.” alisema Sheddy.

Sasabu wengi huwa hawapendi kusema kiwango wanacholipwa, nilipomuuliza kama amelipwa zaidi ya shilingi milioni 1 alijibu;
Sheddy:[kicheko] Inazidi milioni 1 hata milioni 3 inazidi kabisa nimelipwa vizuri

Nikaendelea kumuuliza kama amelipwa zaidi ya shilingi milioni 5?

Sheddy:[kicheko na kigugumizi] labda nisiongelee sana hilo ila nimelipwa pesa nyingi kwakweli nisiwe muongo wala nisiwe mnafiki, mwenyezi Mungu ananiona hata kama nikiongea uongo nimelipwa pesa nyingi SANA (akasisitiza) kiasi cha kwamba ninaweza nikakaa studio kwa muda hata wa miezi miwili au mitatu ndo nikaipata pesa hiyo lakini nimeipata kwa kazi moja na kazi bado sijamaliza na kuwakabidhi bado sijawakabidhi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Kizazaa cha fedha za Kampeni Lowassa, CHADEMA na UKAWA


Kwa mujibu wa habari nyeti nilizotonywa sasa hivi kuna kizazaa cha fedha za kampeni zinazowafanya
Lowassa, Chadema na UKAWA kwa ujumla kuwa katika mtafuruku mkubwa na mpaka sasa uliopelekea kuchelewa kuanza uzinduzi wa kampeni ya Urais wa ukawa.

Vyama vinayounda UKAWA vinasema Lowassa aliahidi kuwa atatowa fedha zote za kampeni kwa hiyo wao wasiulizwe. Lowassa anasema alizotowa zinatosha (hasemi katowa kampa nani na za nini), Chadema nao wanavunga kuwa mpaka sasa akaunti ya kutowa kiasi kikubwa cha fedha ni lazima saini ya Katibu Mkuu iwepo na Katibu Mkuu wa chadema alipofatwa kusaini yeye kagoma ( huu ni ungo wa chadomo) wanasema eti Katibu Mkuu wao anataka kwanza taratibu za kubadili saini yake zikamilike kama watatowa fedha watowe wenyewe akikamilisha zoezi la kubadili kuwa ndiyo anawakwamisha.

Kizungumkuti kinaendelea wakati marafiki matajiri waliokuwa wanampa fedha azitakazo Lowassa wameona mambo yanakuwa magumu na badala ya fedha wameanza kumpa ahadi za kesho, kesho, kesho huku wakitazama upepo unapovuma.

Kuna habari nyingine kuwa kuanzia jana kuna ng'ombe zaidi ya 3,000 wanapakiwa wapelekwe sokoni kutoka kwenye ranchi moja kubwa sana iliyopo huko Handeni, sijuwi nayo inahusiana na Lowassa?

Kwa mujibu wa mtonyaji wangu anasema, Ndesamburo nae kagoma kutowa fedha, anasema Lowassa aliahidi atatowa fedha zote za kampeni yake yeye mwenyewe kwa hiyo asiulizwe yeye.

Mzee Mtei yupo mbioni kuwasiliana na Lowassa, Lowassa hapatikani kwa muda mrefu kwenye simu

Jamii Forums-Written By FaizaFoxy
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Baba Diamond Akataliwa Kumuona Mjukuu wake Tiffah


Baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’.
MSHTUKO! Baada ya hivi karibuni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata mtoto wa kike, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kupitia kwa mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Abdul Jumaa ‘Baba D’ amekataliwa kumuona mjukuu wake huyo, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.

ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa baba Diamond, baada ya Tiffah kuzaliwa Agosti 6, mwaka huu, mama mzazi wa nyota huyo, Sanura Kassim a.k.a Sandra alimpigia simu mzazi mwenzake huyo na kumjuza kwamba wamepata mjukuu, jambo ambalo walilifurahia kwa pamoja.

Wakiwa katika mazungumzo hayo kwenye simu, baba Diamond alimuuliza kuhusu sura ya mtoto kama kweli ni wa kwao au siyo kama tetesi zinavyozagaa kwamba siyo wao ambapo alihakikishiwa na mama huyo kuwa Tiffah ni damu yao kwani anafanana na mtoto wao Diamond hasa mdomo.

BABA DIAMOND AFURAHIA
“Nilifurahi sana nilipopigiwa simu na mama Diamond na kuniambia tumepata mjukuu tulipongezana, pia nikamuuliza kuhusu wasiwasi wa kwamba siyo damu yetu kama wengi wanavyodai ambapo alinihakikishia kwamba ni damu yetu,” alisema baba Diamond.

AKATALIWA KUMUONA, APIGWA CHANGA
Baba Diamond alifunguka kuwa, wakiwa wanaendelea na mazungumzo, alimtaka mzazi mwenzake huyo amwelekeze nyumbani ili akamuone mjukuu wake, Tiffah lakini mama D alimpiga ‘changa la macho’ na kumwambia hawapo wameshasafiri kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

“Niliumizwa sana na maneno hayo kwani yalionesha wazi kwamba, mama D hataki niende kumuona, kwani nyombo vya habari kila siku vinaripoti kwamba Zari na mwanaye wapo hapa Bongo lakini nikaona isiwe shida nikapiga kimya tu,” alisema baba Diamond.
Hata hivyo, baba D alisema kuwa, kutokana na kupigwa changa hilo la macho, hakuweza kwenda kwani hajawahi kufika hata nyumbani kwa Diamond alikohamia huko Madale-Mivumoni jijini Dar na anaona sawa tu kwani hana la kufanya.

UKWELI NI HUU
Kwa mujibu wa mtu wa ndani kwenye familia ya Diamond, ukweli ni kwamba, Zari na mwanaye Tiffah mpaka sasa wako nyumbani kwao na hawajasafiri kwenda Sauz kama alivyoelezwa baba

Diamond mwenyewe hakuweza kupatikana kuzungumzia jambo hilo kwani muda wote simu yake ya mkononi haikupatikana hadi tunakwenda mitamboni.
Source:Globalpublishers
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Siasa yamtia Akili Baby Madaha..Amekata Shauri Kuachana na Skendo na Utoto ili.........


Baby Madaha Katika Pozi
BAADA ya kushuhudia wasanii wenzake wakijiingiza katika siasa na kuanguka, staa wa muziki na filamu, Baby Madaha ametia akili na kusema sasa atatulia kwani ni imani yake siku moja atajiingiza katika jukwaa hilo.

Alisema sasa ameamua kuachana na maisha ya skendo za kila siku kwani aliumizwa sana na madai ya kutumia dawa za kulevya, kitu kilichomuumiza hadi mama yake mzazi.

Ninajiandaa kuwa kiongozi wa kisiasa miaka ijayo, unajua hata wenzetu walioingia kugombea uongozi wa siasa na kushindwa, ilichangiwa na historia ya maisha yao ya kisanii, sisi ni watu wa skendo tu, nimejifunza kitu kutokana na hilo, nimeamua kuacha utoto, sitaki tena skendo,” alisema Baby Madaha.
Source:Globalpublishers
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Updates: Mkutano wa Edward Lowassa na wanawake wa DSM kutoka Ukumbi wa Millenium Tower


Kama tulivyowatangazia jana rais matarajiwa wa awamu ya tano Kamanda mpambanaji asiyechoka na mzee wa maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa atalihutubia Taifa kupitia wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kusikiliza kilio cha wanawake wa Tanzania na atatoa mwelekeo wa UKAWA kwa wanawake na Taifa kwa ujumla baada ya kushika dola mwezi Oktoba.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi saa 8 mchana na utarushwa moja kwa moja na kituo bora cha Televsheni Tanzania cha ITV.

Kati ya wanaotarajiwa kuhudhuria ni wanawake wajasiriamali,mama ntilie,wafanya usafi,akina mama wa nyumbani,wanaoishi katika mazingira magumu,wenye ulemavu na waliojariwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Mgombea huyo wa Urais kupitia UKAWA atakutana na wanawake hao ikiwa ni siku moja tangu serikali ya CCM kumpiga marufuku kukutana na wafanyabiahsra mbalimbali masokoni,wagonjwa mahospitalini na pia kumzuia kupanda daladala.

Wakati Lowassa akitendewa hayo mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu amekuwa akisindikizwa na polisi kutembelea wagonjwa mahospitalini na ni juzi tu alikuwa katika hospitali ya HUruma Mkuu Rombo ambapo alikutana na wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo na kusababisha shughuli katika hospitali hiyo kusimama kwa zaidi ya saa tatu.

Timu ya wanahabari wa UKAWA imeshafika hapa Ukumbini na tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri kabla na wakati wa mkutano.

Karibuni..
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

UKAWA Mnaniharibia Mwanangu, Nakosa Raha Nyumbani Kwangu Mwenyewe


Kila nikitaka kwenda nyumbani kwangu,nasitasita. Natafakari namna na kujibu mapigo ya mpigo toka kwa mwanangu. Kijana wangu huyu aliye Chuo Kikuu,akiwa likizoni sasa,ananitambia na kunibeza katika nyumba yangu mwenyewe.

Najuta kumpa uhuru wa kidemokrasia tangu akiwa Shule ya Msingi. Kila akiniona ananitambia kuhusu UKAWA na kukwama kwetu kama CCM.

Nimejaribu kumwambia kuwa mimi sipo tena kwenye kampeni za CCM. Bado ananing'ang'ania. Ananibakisha CCM na kunihusisha moja kwa moja na kampeni za wagombea wetu kuanzia Dr.Magufuli, Mama Samia, wale wa Ubunge na Udiwani.

Nyumba yangu mwenyewe imegeuka uwanja wa tambo na vikumbo vya kikampeni. Yeye amejipambanua kuwa ni mfuasi wa UKAWA kupitia CHADEMA.

Leo, ameshanipigia simu kujiproud kuwa Lowassa anaibomoa ngome ya CCM pale Millenium Towers. Anadai kuwa Lowassa atawateka wanawake wa Tanzania na kuifanya CCM ibaki na wazee tu kama wapigakura wake.

Akajinasibu kuwa wanawake wa Tanzania wanaiacha mkono CCM na inaelekea kuyumba pamoja ya karata yake ya kumsimamisha Mama Samia kama mgombea mwenza.

Leo pia, amenidokeza kuwa watanzania hawa si wale. Amesema kuwa ana tafiti zilizo fiti zikionesha kuwa UKAWA ndiyo dawa. Ananisubiri anioneshe nikifika nyumbani jioni.

Lengo lake nalijua. Ni kuninyanyasa kisiasa lakini kisasa. Kwa hoja za haja bila kubadili lahaja. Najiandaa,kwa kujisomea nyaraka za haraka na baraka,kwenda kupindua tafiti zake. Nikifika nyumbani, kampeni za chumba kwa chumba zitaanza.

UKAWA mmeniharibia mwanangu. Kwasasa hadi ana kibwagizo chake: MAGUFULI APIGE KAMPENI, LOWASSA ATAPIGIWA KURA! Kazi kwelikweli.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

UKAWA Kutumia Viwanja wa Jangwani Jumamosi


Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene imesema kuwa

Ghafla hiyo itafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa malalamiko yao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI