January Makamba Azomewa Jimboni Kwake


Mheshimiwa January Makamba, Mbunge wa Bumbuli, leo amekumbwa na kitu ambacho hakukitarajia katika maisha yake baada ya kukutana na hasira za wananchi wake jimboni.

Mbunge huyo ambaye sasa yuko katika ziara jimboni kwake kwa zaidi ya siku tano, amekuwa anatembelea baadhi ya vijiji na maeneo katika kutimiza ahadi zake na ilani ya chama chake.

Ziara ya Mh. January ilianza kwa kasoro ambazo wananchi wengi wamekuwa wanaziita usanii, wengi wanalalamikia utaratibu wa ziara zake jinsi unavyoenda, kwanza amekuwa akiitisha mikutano mapema na yeye kutokea akiwa amechelewa, halafu akifika kwenye mkutano hataki kuulizwa maswali wala kuchukua maoni ya wananchi kwa kisingizio cha muda kuisha, katika mikutano yake amekuwa akiongozana na viongozi wa chama wilaya na wale wa halmashauri ambao pia wamekuwa wakitumia ubabe kuendesha vikao na mikutano, viongozi wote wanalazimishwa kumsifia kila wanapopewa nafasi ya kuongea.

Ziara ya Mh. January imekuja baada ya yeye kutoonekana jimboni kwa muda mrefu na wananchi kuona kama aliwatelekeza, wengi wanadai hawajawahi kumuona mbunge toka achaguliwe na leo amekuja kisa kuna uchaguzi unakuja na ameona upinzani umekuwa mkubwa kwa nafasi yake.

Leo Mh. January wananchi wa kata ya Mgwashi ndio waliamua kumtolea uvivu baada tu kufika kwenye mkutano na kuanza kuzomewa na kurushiwa maneno na wananchi, wananchi hawakumruhusu kuongea na walimuambia aondoke hawataki kumuona kwani katika miaka yote mitano aliyokuwepo madarakani amekuwa mbunge wa mitandao na ameshinda kuwa karibu na wananchi waliomchagua, kulitokea vurugu kubwa sana leo mgwashi na viongozi waliokuwa katika msafara wake wengi walipata wakati mgumu sana kutuliza wananchi hao wenye hasira.

Wananchi walimuambia wazi kwamba hawataki kumuona na hajalifanyia jimbo lao lolote zaidi ya kuleta migogoro jimboni na kuwaletea wananchi maisha magumu, vurugu hizi zilidumu mpaka saa 2 usiku na kulikuwa na zomeazomea mpaka mwisho, wananchi wanasema WANATAKA MABADILIKO.

Kuna dalili kubwa sana kwamba Mh. January ana upinzani mkubwa sana jimboni kwake kupitia UKAWA lakini hata ndani ya CCM kwani mpaka sasa wameshajitokeza wagombea wengi kulitaka jimbo hilo, badhi ya wagombea hao ndani ya ccm ni pamoja na mwandishi wa habari wa raisi PREMI KIBANGA, MNEC wa Wilaya Lushoto NAJIM MSENGI na Bwana Abdul Kanik, upande wa UKAWA wengi wanatajwa na kwa hali inavyoendelea UKAWA unaamini una nafasi kubwa kwani umekuwa unakuwa jimboni humo kwa kasi.

Mh. January analalamikiwa kwa kutokuwa karibu na wananchi, uamuzi wake wa kufunga kiwanda cha chai ambacho ndio tegemeo pekee la wakulima kwa sababu za kutoelewana na mwekezaji na uongozi wa kiwanda, kushindwa kutatua mgogoro wa kidini ulionzishwa na baba yake dhidi ya bakwata.

By busaraza2015/JF